Ticker

10/recent/ticker-posts

MICHEZO: Utulivu wa Viongozi wa Yanga Mafanikio Kwa Yanga

Yanga imekuwa na kikosi imara kwa msimu wote wa mashindano, wachezaji wamekuwa na viwango vyenye mwendelezo. Djigui Diarra, Dickson Job, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Fiston Mayele wamekuwa uti wa mgongo wa kikosi cha Yanga.

Benchi la ufundi la Yanga chini ya makocha Nasreddine Nabi na Cedric Kaze, huwezi kutaja mafanikio ya Yanga pasipo kuona umuhimu wa watalaam wanaounda benchi la ufundi. Wamekuwa na utulivu na kucheza kwa mipango.

Viongozi wa Yanga wamekuwa wamoja sana, kwa mfano mchezo wa jana [Marumo Gallants vs Yanga] mwekezaji Ghalib Said Mohamed, Rais wa Yanga Eng. Hersi Said, Makamu wa Rais Arafat Haji, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Seif Khamis Gulamali, wadau wa Yanga Abbas Tarimba, Samuel Luckmay na wengine wote waliungana na kuwa kitu kimoja.

Mashabiki wa Yanga wanaoishi Afrika Kusini lakini wapo waliosafiri kutoka Tanzania kwa pamoja wapo nyuma ya timu yao kuhakikisha inafanya vizuri.

 

Post a Comment

0 Comments