Ticker

10/recent/ticker-posts

MFANYAKAZI AU MJASIRIAMALI JE ? WAJUA KUNA KUSTAAFU?SOMA HAPA UJIPANGE NAMNA YA KUSTAAFU BILA MSONGO WA MAWAZO

 


KUSTAAFU

1. Siku moja utastaafu.

Hautakua ukie

nda kazini, hautakua na madaraka tena, hautakua na nguvu ya ushawishi, mzunguko wako wa pesa utapungua kabisa!

Chunguza/fuatilia tarehe yako ya  kustaafu kwenye risiti yako ya malipo ya mshahara. 

2. Tumia vizuri siku zako za likizo ya Mwaka.

Chochote utakachokifanya Likizo ndio utakachokifanya ukistaafu.Kama unatumia likizo kulala au kuagalia Luninga ndicho utakachokifanya ukistaafu.Tumia wakati wako wa ziada kujifunza kitu, kitakuja kuwa na manufaa ukistaafu.

3. Wekeza kwa ajili ya kustaafu kwako. 

Watoto wako sio uwekezaji kwa ajili ya kustaafu kwako. Usiwategemee watoto, ndugu, au marafiki kama benki yako. Utapoteza heshima na utu wako. 

4.Tafuta shughuli unayoipenda/unayoifurahia wakati bado upo kazini ikuongozee katika kustaafu kwako mfano kufuga kuku au miliki duka pata ujuzi unaojiuza (sio vyeti visivyo na matumizi)

5.Utastaafia wapi?.

Jijengee nyumba. Usistaafu ukiwa bado unapanga nyumba.

Usigome kutoka kwenye nyumba ya serikali.

6.Ni nani watakua wategemezi wako?

⁸Wakati unastaafu watoto wako wanatakiwa wawe wamevuka miaka 18 na wanajitegemea wenyewe.

7.Usistaafu na ukaendelea kukaa katika jiji kubwa 

labda endapo unajimudu kweli kweli, kama Utakua na vyanzo vya fedha hafifu na itakuwia vigumu. Ikiwezekana hamia mahali penye gharama ndogo za maisha ili pensheni yako ikusogeze mbali kidogo.

8.Miliki mali inayoweza kukodishika au inayoweza kubadilika na kuwa Fedha taslimu

Miliki hisa zinazokunufaisha, 

Panda Miti ya biashara mfano mirunda, mitiki, n.k. au fuga, lima mboga mboga ukiweza. Shughuli hizi zitakuingizia mapato pamoja nakukufanya uwe mwenye afya njema.

9.Ishi maisha ya kawaida (maisha yasio na makuu Kama hujajenga nyumba kijijini kwenu, usitumie pesa ya kustaafu kujenga, si busara kufanya hivyo labda kama utageuza kijiji makazi yako ya kudumu.

Tambua kwamba Wastaafu wengi wanakufa mapema kwasababu zifuatazo:-

1.Hawajajiandaa kiakili kustaafu.

2.Kukosa vipato.

3.Msongo wa mawazo.

4.Wanapatwa na shinikizo la juu la damu/kisukari kutokana na  wasiwasi, uoga, n.k

_MEZA YAKO PALE KAZINI SIO YA KUDUMU, JIPANGE KWA AJILI YA KUSTAAFU.

Post a Comment

0 Comments