Ticker

10/recent/ticker-posts

UWT HAI YAPOKEA MIFUKO 20 YA SARUJI TOKA KWA MWENYEKITI UWT KILIMANJARO

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa kKilimanjaro Ndugu Elizabeth Minde (Mwenye Suti Nyeusi)akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Hai Ndugu Happiness Kimaro saruji kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya katibu wa UWT wilaya ya Hai huku akishuhudiwa  na afisa wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Hai Ndugu Petronila Tairo pamoja na maafisa wengine wa CCM  wa wilaya ya Hai na Mkoa wa Kilimanjaro.

Ndugu Happiness Kimaro amesema  Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kupitia umoja wa wanawake wilayani huko wamepokea mchango wa saruji mifuko 20 ikiwa ni mchango kwa ajli ya kujenga ofisi ya katibu wa UWT wilaya ya Hai.Akipokea mifuko hiyo mweneekiti huyo wa  Umoja wa Wanawake Wilaya ya Hai Ndugu Happiness Kimaro amesema makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya CCM wilaya ya Hai ambapo Ndugu. Happiness  Kimaro baada ya makabidhiano hayo alisema,..

''Leo tarehe 4.5.2023 kwa niaba ya   umoja wa wanawake ccm  wilaya ya Hai  nachukua nafasi  hii kushukuru  mwenyekiti wa UWT   mkoa wa Kilimanjaro  Mama Elizabeth Minde. Kwa kutusaidia mifumo 20 ya cement  kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT  wilaya.  Mwenyenzi  mungu akubariki sana pale ulipotoa Mungu akurejeshe..asante  sana...''

Post a Comment

0 Comments