Ticker

10/recent/ticker-posts

RC ROSEMARY SENYAMULE AWATAKA VIONGOZI CHAMWINO KUSIMAMIA KWA UKARIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA

wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewaasa viongozi wa Wilaya ya Chamwino kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa Mradi wa Chuo cha VETA kwa ukaribu ilikuweza kukamilika kwa haraka kama inavyotarajiwa na kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu. 


Mhe. Senyamule amesema hayo leo tarehe 09 Mei 2023 wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Veta Mlowa Bwawani katika Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.

“Niwapongeze Wizara ya Elimu kwa kuchukua hatua haraka na kuanza kutekeleza mradi huu, Mradi huu tofauti yake ni kwamba uliteuliwa kutumika katika uzinduzi kwa niaba ya miradi yote 64 ya vyuo vya Veta vinavyo jengwa Tanzania ndio maana utatakiwa uende kwa haraka ili wakati wa uzinduzi uwe umefikia hatua ya jiwe la msingi “ 


Kwa Upande wake Profesa Carolyne Nombo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema ujenzi wa Chuo hicho unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 6, aidha ametoa wito kwa Watanzania wote kushiriki Kongamano la Elimu ili kujadili mitaala bora ya Elimu ambayo itawasadia Watanzania kujiajiri na kuajiliwa litakofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Mei katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.


Kwa upande mwingine, mmoja ya Fundi anaetekeleza ujenzi wa Mradi huo Bw. Daudi William amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ambayo inawasadia kupata fursa za ajira na kuwapatia fedha kwa ajili kuendesha Maisha ya kila siku.


Post a Comment

0 Comments