Ticker

10/recent/ticker-posts

MHANDISI SEFF: MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA TARURA MKOA WA KILIMANJARO KAZI INAENDELEA

mkuu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (tarura) Mhandisi Victor Seff amesema Ndani ya miaka miwili ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania madarakani hali ya mtandano wa barabara unaosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) umezidi kuimarika na kazi kubwa imefanyika baada ya kuongezeka kwa bajeti.

TARURA Mkoa wa Kilimanjaro unahudumia kilomita 4,659.93 ambapo kilomita 36.40 ni barabara mpya na kati ya hizo Barabara za Lami Kilomita 202.99, Barabara za Changarawe Kilomita 1,198.45 na Barabara za Udongo Kilomita 3,258.49.

Pia kati ya kilomita 4,659.93 za barabara, kilomita 1,767.3 ni za mjumuisho, kilomita 2,250.13 ni barabara za mrisho na kilomita 642.50 ni barabara za Kijamii.

Pia akizungumzia hali ya barabara, Meneja wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Nicholas D. Francis anasema, hali ya barabara zinazohudumiwa na TARURA Mkoa wa Kilimanjaro sehemu kubwa ni nzuri na wastani. Ambapo, kilomita 1442.62 sawa na asilimia 30.96 zipo katika hali nzuri, kilomita 1690.29 ikiwa ni asilimia 36.27 zipo katika hali ya wastani na kilomita 1527.02 ikiwa ni asilimia 32.77 zina hali mbaya.

Mhandisi Francis anasema kuwa kabla ya ongezeko la bajeti TARURA Kilimanjaro ilitengewa bajeti ya Sh bilioni 8.19 kwa mwaka 2020/21 kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

Anasema kwa mwaka 2021/22, TARURA Mkoa wa Kilimajaro ilipata ongezeko la Sh bilioni 13.5 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo Sh bilioni 9.0 ni fedha za Tozo ya Mafuta (Sh. 100 kwa kila lita ya Mafuta ya Dizeli na Petroli) na Sh bilioni 4.5 ni fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali kwa ajili ya Miundombinu ya Barabara (kupitia Majimbo)

Akizunguzia bajeti na kazi zilizofanyikwa ndani ya miaka mwili ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia madarakani kwa kuanza na mwaka 2021/22, Mhandisi Francis anasema kuwa Sh bilioni 18.5 zilitengwa kwa ajili ya bajeti ya miradi maendeleo.

“Aidha, Serikali imekuwa ikituwezesha fedha za miradi ya dharura pale penye uhitaji ili kuweza kufanya barabara ziweze kupitika endapo inatokea uharibifu ambao haukuwekwa katika bajeti.”

Mhandisi Francis anasema TARURA Mkoa wa Kilimanjaro pia ulitengewa na kupokea Sh bilioni 8.222 kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

Post a Comment

0 Comments