Ticker

10/recent/ticker-posts

HILI NDILO ENEO LINAOTAJWA KUWA ZURI ZAIDI KWA SASA JIJINI DODOMA

Malaika Village ni moja ya maeneo mapya kabisa yaliyofunguliwa ambayo yanaongeza uzuri na chachu ya Serikali kuhakikisha jiji la dodoma linakuwa kitovu cha shughuli za serikali ikiwepo kuwa mbele kwa kila jambo bora kulingana na hadhi yake.

Malaika Village iliyopo kilomita mbili tu kutoka njiapanda ya Chamwino na mita chache mkabala na makao makuu ya JKT  tayari imevunha rekodi ya kuwa eneo pekee linalokuwa na ndege urembo wanaofugwa majumbani mfano Njiwa,Kuku,Kanga na wengine ambao pamoja na kuwa kivutio kwa watu mbalimbali wanaofika eneo hilo lakini bado wanatumika kama aina mojawapo ya vyakula vinavyopatikana eneo hilo.


Wakiongea baadhi ya wateja waliopata huduma katika eneo hilo la burudani bwana Juma Mzee mkazi wa Area D dodoma  amesema...Hakika kwa sisi wakazi wa Dodoma tunathubutu kusema hapa malaika village kwa sasa ndio habari ya mjini, mimi na familia napenda kuja hapa mara nyingi weekend kwa sababu kuna Swimming Pool kwa ajili ya watoto ana watu wazima,kuna mandhari tulivu sana hata kama una shughuli zako unafanyia hapa bila kelele na hata makazini tukiwa na vikao tunafanyia hapa.

Naye Juliana Erasto ambaye ni mmoja wa wanafunzi na mfanyakazi wa vyuo vikubwa hapa dodoma amesema..Sisi kwa kweli baada ya pilika pilika za shule kwa wiki au mwezi huwa lazima tuje hapa kupunguza presha ya shule angalau masaa manne aya kuogelea na kuangalia mpira tayari tuna refresh akili na tunarudi upya shuleni tukiwa na utulivu,sisi binafsi tunawashukuru hawa walioleta wazo la malaika village maana hata watu wanaotuhudumia hapa wana uwezo na weledi mkubwa bila kusahau vyakula vyao vinatufanya sisi tunajichanga hata wanne tunakuja tunakula,tunaogelea,tuna relax na kuwa na akili mpya za kusioma mimi ni hayo tu.

Malaika Village unaweza kuwasiliana nao kwa namba 0746 727 662 kwa ajili ya kuweka nafasi yako ya malazi,vyakula au maulizo iwe uko dodoma au unategemea kutembelea jijini dodoma.

Post a Comment

0 Comments