Ticker

10/recent/ticker-posts

MBUNGE SILAA ATAKA BEI YA MAFUTA IONGEZWE JIJINI DAR ES SALAAM,SABABU KUBWA NI HII

Mbunge wa Ukonga Mhe.Jerry Silaa leo 18/04/2022 ameeleza kuwa anapendekeza bei ya Mafuta iongezwe Th.100 kwa lita kwa Jiji la Dar ess Salaam ili iwe sawa na watumiaji wa nishati hiyo wanaokaa mikoa mingine lengo likiwa ni kuliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liidhinishe ongezeko hilo la bei ili Tsh.100 itakayoongezeka kwa kila lita itumike kujenga barabara zote za majimbo ya jiji la Dar es Salaam.

Aidha Silaa ameelezea jinsi ambavyo barabara za jiji la Dar es Salaam zimekuwa kero kwani hata akiwa jimboni kwake akiwa katika majukwaa ya kijamii mfano shughuli za dini (Pasaka au Mwezi Mtukufu) anajikuta akipata maoni au ''Komenti" zinazoonyesha wazi wananchi wa jimbo lake wanahitaji barabara na kero mojawapo kwa wakazi wa ukonga na dar es salaam ni Barabara.

Haya hapa mapenedekezo ya ongezeko hilo toka kwa Mbunge huyo:-

Matumizi ya Mafuta Nchini lita (siku) 10,769,686

(diesel 6,365,578, petrol 4,365,578 na kerosine 37,614) Matumizi ya Dar ni lita 3,399,944 sawa na 31.5%

Bei ya mafuta ;

Dar Tzs 2847 (wastani)

Ngara Tzs 3050 tofauti ni Tzs 203

Tunaomba tozo ya Tzs 100 ya Dar Tutapata 339,994,400 kwa siku.

Tzs 124,097,956,000 kwa mwaka.

Bei ya Dar itakuwa 2947 kama Arusha au Chemba

Kwa kuwa matumizi ya Dar ni 31.5% ya mafuta yote; Serikali itoze Tzs 31.5 kwa kila lita na Ewura wafidie kwenye Bei.

Sikiliza Video Hii Hapa Mbunge Silaa akielezea kwa kina.


Post a Comment

0 Comments