Ticker

10/recent/ticker-posts

Jionee huyu Mwanaume aliyetumia zaidi ya Mil.300 Kwenye Upasuaji wa kurefusha miguu kufikia inchi tano ili kupata mpenzi.

Moses Gibson, 41, wa ene la Minnesota anasema anatatizika kupata rafiki wa kike [girlfriend]kwa sababu ya urefu wake na kabla ya kufanyiwa upasuaji wa kurefusha mguu, aliwahi  kuchukua vidonge ambavyo anasema vilitangaza kwa uwongo kwamba vingemsaidia kukua ndipo aliamua kumtafuta  mganga wa kiroho[spiritual healer] ambaye inasemekana alimwambia inaweza kutokea ikiwa angezingatia urefu wake kwa akili yake yani hayo ni masuala ya kiroho. 

Alifanyiwa upasuaji mwaka wa 2016, ambao uliongeza inchi tatu kwa urefu wake, ukimuacha akiwa na futi 5 na inchi nane. 

     “Baada ya utaratibu wa kwanza, nilifurahia kwa kiasi fulani, lakini ilikuwa akilini mwangu kwamba nilitaka kufanya upasuaji wa pili ili kukamilisha dhumuni lake.

   ’’ Nimepata pesa, na ninaweza kumaliza safari,nyingine” alieleza

   ’’ Nimepata pesa, na ninaweza kumaliza safari,nyingine” alieleza.

Gibson aliweka $98,000 [tsh 222,942,074] ili kufanyiwa utaratibu wa pili Machi mwaka huu na anatarajia kuongeza inchi nyingine mbili kwa urefu wake. 

Hata hivyo, Gibson alitafiti zaidi na kujifunza kama angeweza kukua kwa kufanyiwa upasuajina alihifadhi zaidi ya $75,000 kwa upasuaji huo kwa miaka mitatu kwa kufanya kazi yake ya mchana kama mhandisi wa programs na usiku kama dereva wa Uber na mpaka sasa ameripotiwa kutumia zaidi ya $170,000 [tsh.397,974,760] kwa upasuaji tena wa kurefusha miguu mara mbili ili kumsaidia  kuwa na urefu wa inchi 5 na kumsaidia kujenga imani ya kukubalika  zaidi katika eneo la uchumba.

Wakati wa upasuaji, madaktari walivunja mifupa yake ya tibia na fibula Kisha  kuongeza mfupa ndani yake na zaidi ya hayo, inaruhusu mwili kukuza tishu mpya za mfupa ili kujaza mapengo kwa urefu wake mpya.

    “Wanakupa dawa za maumivu zenye nguvu kwani kuna wakati zinauma sana na lazima ufanyie kazi. Unarudi nyumbani na una wiki moja au mbili kupona kabla ya kupata kifaa kuanza kurefusha.”

Gibson anatumai upasuaji huo utamsaidia kukua na kufikia angalau futi 5 na inchi 11 kwani anatumia kifaa cha kuongeza urefu ili kumsaidia kukua kwa milimita na anasema taratibu hizo zimemsaidia kuzungumza na wanawake na kwa sasa yuko kwenye uhusiano.

Upasuaji wa kurefusha mguu ni utaratibu wa kimatibabu unaoongeza urefu wa miguu ya mtu na Upasuaji huu kwa kawaida hufanywa kwa watu walio na tofauti kubwa ya urefu kati ya miguu yao au tofauti ya urefu wa kiungo kutokana na hali ya kiafya, kama vile dwarfism au jeraha la awali.

Post a Comment

0 Comments