Ticker

10/recent/ticker-posts

WATAKAOLALA NYMBA ZA WAGENI (GESTI) SIKU YA SENSA WATAFUATWA KUHESABIWA


Na Richard Mwaikenda, Dodoma

WATU wote watakaolala nyumba za wageni (Gesti) Siku ya sensa ya Watu na Makazi watafuatwa huko huko na makarani  kuhesabiwa.

Hayo yamesemwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa wakati wa mkutano na wadau wa Mkoa wa Dodoma wa kuhamasisha na kutoa elimu juu ya sensa ya watu na makazi.

"Watu wote watakaokuwa wamelala siku hiyo Guest, hotelini  makarani watakwenda kuwahesabu ikwemo na wale wote watakao safiri maeneo mbalimbali," amesema Dkt Chuwa.

Amesema kuwa siku hiyo  usiku majira ya saa 6 na dakika moja makarani wa sensa wataanza kuhesabu kwenye Gesti, mahotelini, stendi na maeneo mengine yanayohusisha safari.

Aidha, Dkt. Chuwa amesema kuwa wageni wote kutoka mataifa mbalimbali ambao siku hiyo ya sensa watakuwa wamelala nchini watahesabiwa na kuchambuliwa baada ya sensa kujua idadi yao na idadi kamili ya wazawa.

Amesema kuwa,licha ya sensa hiyo kuhesabu watu wakiwemo wenye aina mbalimbali za ulemavu, watoto wa mitaani, lakini pia itagusa sekta nyingi kama vile makazi ya watu zikiwemo nyumba na aina mbalimbali za mifugo.

Mkutano huo wa wadau ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Mkoa huo, Anthony Mtaka ulihudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Wengine ni Kamishna wa Sensa, Spika mstaafu, Anne Makinda, wabunge wa mkoa huo, wakuu wa wilaya, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa mabaraza ya wazee na taasisi mbalimbali wakiwemo watu wenye ulemavu.

Sensa WATAKAOLALA GESTI  SIKU YA SENSA WATAFUATWA KUHESABIWA itafanyika Agosti 2022 na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania,  Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments