Ticker

10/recent/ticker-posts

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel Aongoza Kura za Maoni CCM Jimbo la Siha....Agrey Mwanry Kashika Nafasi Ya Pili

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel ameongoza kura za maoni katika Jimbo la Siha, Kilimanjaro kwa kupata kura 148.

Dkt. Mollel amefuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Tabora, Agrey Mwanry mwenye kura 147 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Tumsifu Kweka aliyepata kura 53.