Ticker

10/recent/ticker-posts

ZOEZI LA UANDIKISHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA LAANZA RASMI TANDAHIMBA,WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI

Zoezi la Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Wilaya ya Tandahimba limeanza rasmi huku wananchi wakionekana kuhamasika na zoezi Hilo kwa kujitokeza kwa wingi katika maeneo tofauti Wilayani hapa

Akizungumza katika kituo Cha Uandikishaji Nambahu Afisa Mwandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo la Tandahimba Said Msomoka alieleza kuwa amefarijika kuona  wananchi wamehamasika na zoezi Hilo

Aidha aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura 

Zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura Wilayani Tandahimba limeanza rasmi na linatarajia kumalizika jumapili wiki hii.
 Mwananchi akiwa anafurahi kupata kadi yake ya kupiga kura

 Wanachi wamejitokeza kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
Wananchi wakisubiri kujiandikisha


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NkVbkm
via

Post a Comment

0 Comments