Ticker

10/recent/ticker-posts

TAEC YAELEZA SABABU ZA KUPIMA MIONZI KATIKA MNYORORO WA BIDHAA .



Na.Vero Ignatus.

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imeshiriki katika maonesho ya elimu na biashara yaliyofanyika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar kwa mara

ya pili Kisiwani Unguja ambapo maonyesho hayo huandaliwa maalumu kila mwaka katika kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi ya serikali ya Zanzibar ambapo mwaka huu imeadhimisha miaka 56 tangia mwaka 1964

Maonesho hayo ya siku kumi (14) yalianza rasmi tarehe 02 Januari, 2020, ambapo yalizinduliwa rasmi tarehe 07 Januari, 2020 na Mhe. Zubeir Ali Maulid, Spika wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo kilele chake ni tarehe 15 Januari, 2020 ambayo yamwratibiwa na TAN TRADE na kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Aidha TAEC imekuwa ikishiriki katika maonesho hayo maalum ili kutoa elimu juu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali kisheria ndani ya TAEC ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku lengo kuu likiwa ni kusikiliza na kujibu changamoto za wafanyabiashara na utaratibu mzima wa utolewaji wa vibali vya uingizaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi.

Katika maonyesho hayo TAEC imeainisha sababu mbalimbali muhimu za upimaji wa bidhaa katika mnyororo wa chakula ambapo wananchi na wafanyabishara wameelezwa juu ya sababu za upimaji wa bidhaa hizo, ikiwa ni pamoja na udhibiti wa mionzi katika mnyororo wa bidhaa ili kulinda watanzania dhidi ya madhara hatari yanayoweza kusababishwa na mionzi

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman, alipotembelea banda la TAEC alijulishwa juu ya takwa la kisheria la kupima mionzi kwenye mnyororo wa bidhaa kama ilivyoahinishwa kwenye Sheria Na. 7 ya Mwaka 2003, kuwa Sheria hiyo inaendana na matakwa ya kimataifa ikiwemo

shirika la afya duniani (WHO), shirika la kilimo na chakula duniani (FAO), na shirika na nguvu za atomu duniani (IAEA) katika kuhakikisha mionzi kwenye mnyororo wa bidhaa inadhibitiwa ili kuzuia madhara ya mionzi yanayoweza kujitokeza.

Wakati huo huo Mhe. Bi. Harusi ameitaka TAEC kufika katika Hospitali ya Mnazi mmoja ambayo kwasasa wako katika hatua za mwisho za kufunga mashine za CT-

Scan ili kufanya ukaguzi kabla ya hatua hizo kukamilika. Mhe alijibiwa ya kuwa hatua za awali za ukaguzi zilifanyika na zoezi lingine litaendelea mara mashine hizo zitakaposimikwa.

TAEC pia imeweza kutoa elimu kwa Wananchi na wafanyabiashara waliotembelea banda hilo katika maonyesho hayo juu ya uwepo wa mionzi katika mazingira kutokana na uwepo wa madini ya urani nchini Tanzania ambapo ni sababu nyingine ya msingi iliyopelekea TAEC kulazimika kupima mionzi katika mnyororo wa bidhaa ili kuhakikisha bidhaa zote ziko salama dhidi ya chembechembe au viasili vya mionzi.

Sambamba na hayo wananchi wamejulishwa kuwa wajibu mkubwa wa serikali ni kulinda wananchi, hivyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina wajibu wa kulinda wananchi wake dhidi ya madhara yatokanayo na mionzi, ndiyo sababu imechukua hatua za kulinda mnyororo mzima wa chakula ili wananchi wake wabaki kuwa salama.

Wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya biashara iliyozinduliwa tarehe 10 Januari, 2020 na Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara, Wananchi walijulishwa changamoto mbalimbali za kibiashara zinazojitokeza duniani kwamba Serikali iliamua kuchukua jukumu la kulinda soko la bidhaa zinazouzwa nje ya Tanzania hasa wakati huu wa vita ya kiuchumi

Hivyo basi serikali iliamua kuchukua jukumu la kwa kuzipima na kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kuzisafirisha ili isije kutokea kwa namna yoyote ile watu wasio waaminifu wakazichafua kwa makusudi ili bidhaa zisipate soko, hivyo upimaji wa mionzi katika bidhaa za hapa nchini unatoa uwezekano wa kufuatilia kama kuna shida yoyote na kuchukua hatua zaidi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2FMbpio
via

Post a Comment

0 Comments