Ticker

10/recent/ticker-posts

SOKO LA MAZAO YA KILIMO KUJENGWA LONGIDO


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (kulia) akiongea kuhusu kuanzisha ushirikiano na Halmashauri ya Wilaya ya Longido kujenga soko la mazao ya kilimo katika mpaka wa Namanga.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe.Frank Mwaisombe leo jijini Dodoma
Baadhi ya Watendaji wa wizara ya Kilimo walioshiriki kikao cha Katibu Mkuu na uongozi wa Wilaya ya Longido.

****************************

Dodoma

Wizara ya Kilimo inatarajia kuanzisha ushirikiano na Wilaya ya Longido kwa ajili ya kufanya uwekezaji na uendelezaji wa eneo la kilimo lenye ukubwa wa ekari 50 katika mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga.

Kauli hii imetolewa leo (11.01.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe alipofanya kikao na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Frank Mwaisombe ofisini kwake jijini Dodoma.

“Ni wajibu wa wizara ya kilimo kuhakikisha mazao ya kilimo yanapata soko la uhakika na kuongezwa thamani ili kuwanufaisha wakulima,hivyo uwepo wa soko la mazao
mpakani Namanga utasaidia serikali kuongeza mapato” alisema Mhandisi Mtigumwe.

Katibu Mkuu huyo alisema wizara kwa kuanzia itatuma wataalam kwenda Longido wiki ijayo ikiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko kuweka mpango mahsusi wa
kuwezesha serikali na wawekezaji kutumia eneo hilo la kilimo.

Aliongeza kusema kuwa wizara ya Kilimo kupita ushirikiano hu inataka kuona eneo hili la mpakani linakuwa kituo kikuu cha uwekezaji kwenye kilimo,kwani ni jukuma la wizara kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima kupata masoko ya mazao yao.

“ Wataalam wakae chini baada ya kutembelea Longido na kuweka mpango wa uanzishwaji soko na maghala kwa ajili ya mazao ya kilimo mapema” alisisitiza KatibuMkuu huyo. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisombe aliyeongozana na wataalam wa kilimo na ardhi wa halmashauri alisema ushirikiano na wizara ya kilimounahitajika ili kujenga soko,maghala na viwanda vitakavyoongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa.

Mwaisombe alisema uwepo wa soko na viwanda vya mazao ya kilimo mpakani Longido kutawanufaisha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao kwa bei nzuri na nchi
kupata pato zaidi.“Tunayo fursa nzuri ya kushirikiana na wizara hii kuimarisha masoko ya mazao ya kilimo kabla hayajauzwa nje ya nchi,hivyo kuboresha maisha ya wakulima kama
anavyoelekeza Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli” alisema Mkuu wa Wilaya ya Longido.

Wilaya ya Longido iliyoanzishwa mwaka 2016 ipo mpakani na nchi ya Kenya ambapo kwa mwaka zaidi ya shilingi Bilioni 54 zinakusanywa kama mapato toka ushuru
hususan mazao ya kilimo.Aliongeza kusema Halmashauri ya Longido hukusanya kati ya shilingi milioni 300 kwa mwezi toka ushuru na tozo mbalimbali mpakani hapo,hivyo uwepo wa soko la kilimoutasaidia kuongeza wigo wa mapato toka mazao ya kilimo yanayopitishwa kwa wingi mpakani kwenda Kenya na Somalia.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo aliyataja mazao ya kilimo yanayongoza kupita mpaka wa Namanga kuwa ni mahindi,vitunguu,nyanya na mazao ya mbogamboga na
matunda mengi yakiwa hayajaongezwa thamani.

Kikao hiki kimefuatia ziara aliyoifanya Katibu Mkuu Mhandisi Mtigumwe kutembelea halmashauri ya Longido mwanzoni mwa mwaka huu 2020 kwa mwaliko wa Mkuu wa wilaya hiyo Frank Mwaisombe ili kuona namna wizara itakavyosaidia kutumia fursa ya mpaka kukuza masoko ya mazao ya kilimo kwa manufaa ya wakulima nchini.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2R4TTew
via

Post a Comment

0 Comments