Ticker

10/recent/ticker-posts

Mtawala wa muda mrefu Oman, Sultan Qaboos afariki akiwa na umri wa miaka 79


Sultan Qaboos bin Said Al Said of Oman, mtawala wa muda mrefu katika nchi za kiarabu ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Sultan alimng'oa madarakani baba yake katika mapinduzi ya amani kwa ushriikiano na Uingereza mwaka 1970 na kuiweka Oman katika mwanzo mpya wa maendeleo kwa kutumia utajiri wake wa mafuta.

Alikuwa maarufu sana na mfalme wa nchi hiyo, na yeyote aliyejitokeza kumpinga alinyamazishwa.Sababu za kifo chake bado hazijathibitishwa.

Binamu yake Haitham bin Tariq Al Said ameapishwa kama mrithi wake.

Aliyekuwa waziri wa utamaduni na thurathi za kitaifa ameapishwa leo Jumamosi baada ya mkutano wa Baraza la Familia ya Kifalme, serikali imesema.

Sultan ndo mwenye kufanya maamuzi nchini Oman. Pia anashikilia wadhifa wa waziri mkuu, amiri jeshi mkuu, waziri wa ulinzi, waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje.

Mwezi uliopita, Sultan Qaboos - ambaye hakuwa na mrithi ama mtu aliyekuwa ameteuliwa kuchukua nafasi yake - alikuwa nchini Ubelgiji kwa wiki nzima akipata matibabu na kulikuwa na taarifa kwamba anaugua saratani.

"Kwa huzuni na masikitiko makubwa...familia ya kifalme inaomboleza kifo cha Mfalme Sultan Qaboos bin Said, ambaye alikufa Ijumaa," taarifa kutoka familia ya kifalme imesema, na kutangaza siku tatu za maombolezo.

Picha zilionyesha kundi la wanaume waliokusanyika nje ya msikiti mkuu wa Sultan Qaboos mji mkuu wa Muscat, ambapo jeneza lake limepelekwa kwa ajili ya maombi maalum. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2NddV5e
via

Post a Comment

0 Comments