NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWAITA WAWEKEZAJI DODOMA, AWATAKA KUCHANGAMKIA MAENEO YA UWEKEZAJI

  Masama Blog      
Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara, wawekezaji na wadau wote wa maendeleo ambao wanawekeza nchini ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira rafiki kwao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Mhe Anthony Mavunde alipokua akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Kampuni ya Admire inayofanya biashara ya mafuta mikoa mbalimbali nchini.

Mhe Mavunde amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli inathamini wawekezaji kutokana na mchango wao katika kutoa ajira na kukuza pato la Taifa kupitia kodi wanazolipa.

" Niupongeze uongozi wa Kampuni hii kwa kukuona umuhimu na ulazima wa kuja kuwekeza katika Jiji la Dodoma kwani kufanya hivyo kutaongeza fursa kubwa za ajira kwa vijana ikizingatiwa tayari mmeshatia ajira 20 mpaka sasa kwa wananchi wa Dodoma.

Sisi kama Serikali tunaendelea kutoa wito kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza katika Jiji hili ambalo ndio Makao Makuu ya Serikali lakini pia kuna maeneo mengi ya Uwekezaji na rafiki kwa ajili ya kujenga viwanda, hoteli na hata majengo ya kibiashara, " Amesema Mhe Mavunde.

Kwa upande wake Msemaji wa Kampuni hiyo, Mohammed Ibrahim ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji jambo ambalo linaongeza ari kwao ya kuzidi kufanya Uwekezaji katika maeneo mengi zaidi nchini.

" Kwa kweli serikali ya Rais Magufuli imetoa mazingira rafiki sana kwa wafanyabiashara hasa wazalendo. Sisi tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali yetu ili kufikia ndoto ya Rais wetu ya Tanzania ya viwanda.

Tunafahamu lengo la kila mfanyabiashara ni kuwekeza na kupata faida lakini kampuni yetu ya Admire moja kati ya malengo yake makubwa ni kugawa ajira kwa akina Mama na vijana wengi nchini, " Amesema Ibrahim

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Mhe Anthony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Mafuta ya Admire jijini Dodoma leo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Vijana, Mhe Anthony Mavunde akikata utepe kuashiria kufungua ofisi za Kampuni ya Mafuta ya Admire jijini Dodoma leo..
 Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampuni ya Mafuta ya Admire leo jijini Dodoma.
 


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37CxWKv
via
logoblog

Thanks for reading NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWAITA WAWEKEZAJI DODOMA, AWATAKA KUCHANGAMKIA MAENEO YA UWEKEZAJI

Previous
« Prev Post