MSANII HARMONIZE ACHANGIA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA,DC AMPONGEZA

  Masama Blog      

Mama yake Rajab Abdulkahari a.k.a Harmonize aitwaye Habiba Chivalavala akikabidhi mashuka kwa DC wa Tandahimba Sebastian Waryuba kwa ajili ya hospital ya Wilaya
 Mkuu wa Wilaya  Sebastian Waryuba (katikati)akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Wilaya Omary Nang'uta na Mama Harmonize
 Wananchi ambao walijitokeza katika makabidhino hayo wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Tandahimba Hawa Ramadhani(CCM  viti maalum)
Mashine ya kusaidia kupumua kwa wagonjwa  ambayo imetolewa na Msanii Harmonize.


Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amepokea mashine ya kupumulia na mashuka vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 10 kutoka kwa Msanii Rajabu Abdulkahari (Harmonize)

Vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa na mama yake Habiba Chivalavala amesema vitasaidia wagonjwa katika hospitali ya Wilaya

"Tunashukuru kwa vifaa hivi ambavyo ni muhimu kwa wagonjwa mashuka 48 na mashine ya kupumulia,nami nawakabidhi idara ya Afya ili vikatumike,amesema Waryuba,"

Naye mama Harmonize amesema kuwa  anafarijika kwa mwanaye kurudishia kile anachokipata kwa wananchi hususan huku ambako amezaliwa

"Nafarijika nikiona anatambua umuhimu wa kuwakumbuka  wengine hususan hospital sehemu ambayo haikwepeki,"amesema mama Harmon
ize


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2sFwQyK
via
logoblog

Thanks for reading MSANII HARMONIZE ACHANGIA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA,DC AMPONGEZA

Previous
« Prev Post