BONANZA LA AFYA KWANZA LA DICK PUB VETERANS NA MTI PESA – KIJICHI LAFANA LEO JIJINI DAR

  Masama Blog      
Winga wa MTI PESA akijaribu kumtoka Mlinzi wa Timu ya DICK PUB VETERANS katika bonanza leo katika Uwanja wa Jeshi la Polisi uliopo Mtoni Kijichi, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Dick Pub Veterens wakifuatilia Bonanza hilo(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Kituo cha Polisi chang’ombe, ASP. Dastan Kombe(katikati) ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita, Linus Bwegoge.
Timu ya DICK PUB VETERANS ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya MTI PESA
Timu ya MTI PESA ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya DICK PUB VETERANS.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kati ya DICK PUB VETERANS na MTI PESA wakimenyana katika bonanza leo katika Uwanja wa Jeshi la Polisi uliopo Mtoni Kijichi, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

*************************************

Na Lucas Mboje, Mtoni Kijichi

TIMU ya mpira wa miguu ya MTI PESA ya Mtoni Kijichi, Temeke imefungwa bao tatu(03) na timu ya Veterans ya Dick Pub Klabu ambayo inaundwa na Maafisa wa Jeshi la Polisi,

Magereza, Uhamiaji na majirani wa Kambi ya NASACO Kijichi. Bonanza la michezo huo lijulikanalo kwa jina la ‘Afya Kwanza’ lililofanyika katika viwanja vya Jeshi la Polisi vya Kambi ya Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam limefanyika leo kuanzia majira ya saa 2:00 asubuhi hadi 4:00 asubuhi na kuhudhuriwa na Maafisa, wakakaguzi, askari, wakazi jirani wa Kambi ya Mtoni Kijichi na Familia zao.

Mgeni rasmi katika Bonanza hilo alikuwa ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi ambaye pia ni Ofisa wa Jeshi la Magereza, ACP. Jaka Kizitoambapo amepongeza waandaaji na washiriki katika Bonanza hilo ambalo lengo lake kuu ni kujenga Afya na mahusiano kupitia michezo.

“Niwapongeze sana waandaaji wa Bonanza hili kwani naamini litasaidia katika kuimarisha mazoezi ya mwili hivyo kuboresha afya za washiriki”, alisisitiza ACP. Jaka.

Akizungumza katika Bonaza hilo Mkuu wa Kitengo cha Michezo wa Jeshi la Polisi Tanzania, ACP. Jonas Mahanga ambaye pia ni miongozi mwa wachezaji wa Dick Pub Veterans Klabu amesema kuwa michezo ni moja ya nyanja zinazotumiwa na Jeshi la Polisi Tanzania na Duniani kwa ujumla katika kuwakutanisha watu wenye nyadhifa mbalimbali na kujadili mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu katika jamii ya eneo husika.

Pia ameongeza kuwa michezo ni sehemu ya ajira endelevu ambayo vijana wengi wenye vipaji huajiriwa na kupata vipato halali ambavyo vinawasaidia kukuza uchumi kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

“Nashauri utaratibu huu wa mabonanza uendelee kwa ajili ya kufikia malengo yaliyotarajiwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama litaungana na waandaaji wa mabonanza haya ili yaendelee kufanyika kwa ufanisi mkubwa”, alisema ACP. Jonas.

Wakati huo huo, ACP. Jonas Mahanga katika kuunga mkono mwendelezo wa mabonanza hayo ametoa mpira mmoja kwa timu ya Dick Pub Veterans Klabu na kuahidi kutoa mpira mmoja kwa timu ya MTI PESA.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36mdcGq
via
logoblog

Thanks for reading BONANZA LA AFYA KWANZA LA DICK PUB VETERANS NA MTI PESA – KIJICHI LAFANA LEO JIJINI DAR

Previous
« Prev Post