Ticker

10/recent/ticker-posts

Ibada ya Shukrani ya Prof. Mark Mwandosya kutimiza miaka 70


Wiki iliyopita, tarehe 28 Desemba 2019 nilitimiza miaka 70 tangu kuzaliwa. Kwangu kufikia umri huo ni kwa kudra na rehema za Mwenyezi Mungu. Hivyo basi tulikuwa na Ibada ya shukrani hapo kijijini Lufilyo, Busokelo iliyoongozwa na Baba Askofu Ambele Mwaipopo wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Ziwa Tanganyika na Baba Askofu Panja wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini, wakisaidiwa na Baba Mchungaji Mwasanguti wa KKKT Dayosisi ya Konde, Jimbo la Kati.

Ibada ilihudhuriwa na wananchi na wageni waalikwa kutoka Rungwe, Busokelo, Kyela, Dar es Salaam, Arusha Singida na Kigoma, na Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Rungwe na Busokelo.
 
 Walikuwepo pia wageni kutoka Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Uingereza na Ujerumani na baadhi ya Walimu walimfundisha Prof. Mark Mwandosya Shule ya Sekondari ya Malangali zaidi ya miaka 50 iliyopita.

Pichani kutoka kulia ni wafuatao:Mhe. Balozi Chirau Ali Mwakwere, aliyekuwa Balozi wa Kenya nchini na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Kenya; Baba Mchungaji Mwasanguti; Mwalimu Charles Muhitira aliyenifundisha Historia na Hisabati kidato cha kwanza na cha pili; Mwalinu Clement Bendera aliyenifundisha Kemia, Fizikia na Jiografia kidato cha tatu na cha nne; Baba Askofu Ambele Mwaipopo wa KKKT Dayosisi ya Ziwa Tanganyika; Mwalimu Ambangile Mwakilembe aliyenifundisha Kiswahili kidato cha nne; Mimi; Mama Lucy Mwandosya; na Baba Askofu Panja wa Kanisa la Moravian, Jimbo la Kusini.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2ZIYfLY
via

Post a Comment

0 Comments