Ticker

10/recent/ticker-posts

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA,MIFUGO, NA UVUVI WAKUTANA NA MKUU WA MKOA MARA, WAFANYA KIKAO KIZITO CHA KIMKAKATI

Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Kighoma Malima amepokea ugeni wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Waziri wa Viwanda na Biashara na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhesh. Joelson Mpina alifanya ziara ya siku moja na katika mkutano wake na Mkuu wa Mkoa, Adam Malima alimshukuru na kumkumbusha kwamba mkoa wa Mara ni mdau mkuu wa sekta za mifugo na uvuvi, na kwamba wananchi wake ni wanufaika wakuu wa hatua zinazochukuliwa na Serikali hii ya awamu ya tano.

 Aidha Mhesh. Malima alimuomba Waziri kwamba Wizara na Mkoa zifanye kazi kwa pamoja ili kufanikisha mpango wa mkoa wa kuboresha ngombe na mifugo ya mbuzi na kondoo ili ikidhi mahitaji ya soko kwa maana ya uzalishaji wa nyama na maziwa na mazao mengine yatokanayo. Kwa upande wa Uvuvi RC MARA amemuomba WMUV ushirikiano wa Wizara yake ili kufanikisha doria za ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika ziwa kuu ambapo Uvuvi unafanyika bila usimamizi. 

Waziri alipata nafasi ya kutembelea kiteule cha Jeshi la Wanamaji cha JWTZ ambapo alipata nafasi ya kushuhudia utayari wa wapiganaji wetu wa kulinda rasilimali za Taifa. WMUV aliridhia pendekezo la mkoa na kushauri Kamati ya pamoja ya kutathmini hatua zitakazofuata. WMUV alishauri pua kuwa Kamati hiyo ikae chini ya Uenyekiti wa RAS MARA na akwapa siku saba ya kukamilisha kazi hiyo, ili iwakilishe taarifa yake kwa RC MARA ambaye nae ataiwakilisha kwa WMUV na mamlaka zingine husika.

Baada ya ziara hiyo ya WMUV, RC MARA akapokea ugeni wa Mhe. Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara. WVB alifika Musoma kukutana na Wafanyakazi waliokuwa kiwanda cha MUTEX ambao walipewa likizo isiyokuwa na malipo mwaka 1994 na hawajalipwa mafao yao hadi kipindi hiki, ili kupata maoni yao kuhusu mwenendo uliopelekea Kiwanda hicho kufikia hatua ya kupunguza wafanyakazi na kusimamisha uzalishaji wakati ikiwa chini ya usimamizi wa Sekta ya Umma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Bashungwa aliwahakikishia wadau wote wa sekta za Viwanda na Biashara kwamba Serikali ya awamu ya tano imekusudia kurejesha uzalishaji wa kiwanda cha MUTEX na ipo katika hatua za kupata Mwekezaji mwenye nia na uwezo wa kufanya uzalishaji unaoendana na matumizi ya Pamba itokanayo mkoa wa Mara kama mali ghafi ya kiwanda. WVB aliaahidi kurejea kabla ya kuanza kikao cha Bunge cha Januari 2020 ili kufanya kikao na wafanyakazi wa MUTEX kujadili madeni yao. RC MARA alimshukuru Waziri wa Viwanda na Biashara kwa mapenzi yake kwa mkoa wa Mara na wanaMara.

Awali, kabla ya ziara za Mawaziri RC MARA alimpokea Naibu Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake ambapo Naibu Kamishna Mkuu alimshukuru RC MARA kwa kazi inayofanywa na uongozi wa Mkoa wa Mara katika kuongeza ukusanyaji wa kodi juu ya malengo. Aidha Mkuu wa Mkoa amemeuahidi Naibu Kamishna Mkuu TRA kwamba Serikali ya Mkoa itaendelea kuhamasisha ulipaji wa kodi miongoni mwa wafanyabiashara wa Mkoa wetu.

Akiongelea siku ya leo 11/12 , RC MARA alisema anatarajia matokeo ya ziara hizo zitakuwa za mchango mkubwa kwa mikakati ya mkoa wa Mara ya kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayotokana na mazingira wezeshi yanayojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais JPM.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Kighoma Malima akimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alipokuwa akimueleza jambo
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Kighoma Malima akifafanua jambo kwa
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhesh. Joelson Mpina alipowasilia mkoani humo jana




  Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Kighoma Malima akifafanua jambo kwa
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhesh. Joelson Mpina alipowasilia mkoani humo jana
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Kighoma Malima akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa  alipowasilia mkoani humo jana
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Kighoma Malima akizungumza na
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhesh. Joelson Mpina alipowasilia mkoani humo jana



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/36k6MY2
via

Post a Comment

0 Comments