Ticker

10/recent/ticker-posts

TVP washinda tuzo ya utengenezaji wa makala ya video bora barani Afrika


 Kampuni ya True Vision Production (TVP) imeshinda tuzo ya utengenezaji wa filamu bora barani Afrika (The International Tourism Film Festival Africa (ITFFA). Sherehe za kukabidhi tuzo hizo zinategemewa kufanyika mwakani mwezi Aprili nchini Afrika ya Kusini.

Washindi wa tuzo mbalimbali ikiwemo TVP walitangazwa hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini wakati wa Tamasha la Kimataifa la Filamu lenye lengo la kukuza utalii barani Afrika.
 Waandaaji wa tuzo hizo wameipatia TVP tuzo mbili kupitia video inayoongelea uzuri wa hifadhi ya Ngorongoro nchini. 

Tuzo moja ni kwa video hiyo kushinda nambari moja miongoni mwa video nyingine zilizowasilishwa na kampuni mbalimbali zinazotengeneza filamu barani Afrika na tuzo nyingine ni ya jumla iliyoipa ushindi wa kuwa tuzo nambari moja Afrika katika kipengele cha Uzuri wa Asili na Maisha ya Wanyama mbugani ( Nature & Wildlife). Waandaaji wa tuzo hizo tayari wametuma vyeti vya ushindi wa washindi
Akiongelea vyeti hizo vilivyosainiwa na Mkurugenzi wa Tuzo hizo, Caroline Ungersbock, Mkurugenzi wa TVP, David Sevuri amefurahia ushindi huo, akisema umetokana na weledi wa TVP katika kuzingatia utengenezaji wa filamu bora kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Hii ni mara ya kwanza kutolewa kwa tuzo hizo. Mkurugenzi wa tuzo hizo, Ungersbock amewasifu washindi wa tuzo hizo, ikiwemo TVP huku akisema anategemea ushiriki wao zaidi katika tuzo za mwakani.

Miongoni mwa waliotengeneza filamu hiyo ya TVP inayopatikana YouTube kupitia https://www.youtube.com/watch?v=Fyjieak8lUw  ni pamoja na  Stephano Lihedule ( Producer& Editor), Dickson George ( Cinematographer) na Leonard Ndegeulaya ( Music Composer).

Miongoni mwa washindi wengine wa tuzo hizo ni kampuni ya The Spirit of Kenya walioibuka washindi wa kwanza katika kipengele cha Adventure Tourism wakati washindi wa pili walikuwa kampuni ya The Powerful Soul Of Hongkong

Tamasha hilo la ITFFA lilifanyika mjini Cape Town na Northern Cape. Uoneshwaji wa filamu zilizoshinda ulifanyika mjini Northern Cape katika jumba la maonyesho la Apollo ( Theatre) lililopo Magharibi mwa mji wa Victoria.

Lengo la tuzo hizo ni kutangaza utalii barani Afrika kupitia utengenezaji wa filamu. 
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na TCI, watu milioni 80 mwaka jana walitembelea vituo vya utalii mbalimbali duniani kwa ushawishi walioupata kupitia filamu walizoziangalia, ndio maana wazo la kuwa na tuzo hizi likaja ili kutangaza utalii wa Afrika.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/37i0ZCW
via

Post a Comment

0 Comments