MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA YAANIKA MIPANGO YAKE YA KUIBORESHA BANDARI YA MBAMBA BAY

  Masama Blog      

Baadhi ya mitambo inayomilikiwa na Kampuni ya Godmwanga Gems Ltd yakiendelea kuchimba madini ya makaa ya mawe katika eneo la Malini wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Shehena ya makaa ya mawe yakiwa yamehifadhiwa baada ya kichimbwa na Kampuni ya Godmwanga Gems Ltd .Makaa hayo yanatarajiwa kusafirishwa kwa kutumia usafiri wa majini kupitia bandari za Ziwa Nyasa.
Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Abedi Gallus akizungumza mikakati ya kuboresha bandari ya Mbamba Bay ili kuhakikisha shehena ya mizigo ya makaa ya mawe inapitishwa hapo.
Meneja wa Kampuni ya Godmwanga Gems Ltd Mhandisi Imani Masawe akizungumzia umuhimu wa kuboreshwa kwa miundombinu ya bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Meneja wa Bandai za Ziwa Nyasa (aliyesimama katikati) Abedi Gallus akipata maelezo kuhusu shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe katika kijiji cha Malini wilayani Nyasa .Na Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii-Nyasa

SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imedhamiria kufungua ushoroba wa Mtwara kupita bandari ya Mbamba Bay ambapo tayari imeshaweka miundombinu wa brabara hadi mbinga na iatarajiwa kwamba mpaka kufikia mwaka 2020 kipande cha lami cha kilometa 67 kutoka Mbinga hadi Mbamba Bay kitakuwa kimekamilika ambapo mpango huo unakwenda sambamba na upanuzi wa bandari ya Mbamba Bay.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Abedi Gallus wakati anaelezea mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)ilivyodhamiria kuimarisha miundombinu ya usafiri na hasa usafiri wa maji ambapo amefafanua tayari TPA imeweka mkandarasi mshauri kwa ajili ya kushauri namna ya kuendeleza bandari hiyo ya Mbamba Bay.

Amesema kufunguka kwa ushoroba(njia) wa Mtwara kutapunguza umbali wasafirishaji wa Malawi kwa takribani kilometa 450 kutoka bandarini.Ametoa mfano umbali kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi mji wa Lilongwe ni kilometa 1700 ila kwa kupitia ushoroba wa Mtwara umbali huo unapungua hadi kufikia kilometa 1250. "Tunaipongeza Serikali kwa hatua ambazo inachukua kuboresha bandari za Ziwa Nyasa ikiwemo bandari ya Mbamba Bay ambayo kwetu ni muhimu sana."

Ametumia nafasi hiyo kuwaomba abiria na wasafirishaji wa shehena kutumia miundombiu ya meli a bandari ili kujipatia huduma nzuri kwa gharama nafuu.

Akizungumzia zaidi bandari ya Mbamba Bay, Gallus amesema pamoja na kusafirisha abiria, bandari hiyo ni muhimu kwa kusafirisha makaa ya mawe, na hivi karibuni kumeanza kuchimbwa makaa ya mawe katika Wilaya ya Nyasa eneo la Mbamba Bay na matarajio ya TPA ndani ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 wataanza kusafirisha tani 5000 za mkaa wa mawe kutoka Mbamba Bay kuelekea Malawi na kutoka Mbamba Bay kuelekea bandari ya Kiwira.

"Kwa kifupi tu katika mipango ya TPA tunampango wa kuendeleza bandari hii na kwa sasa tumeshaanza kufanya upembuzi yakinifu kwa kujua ukubwa miundombinu ambayo itawekwa katika bandari hii.

Kuhusu shehena ya mizigo, Gallus amesema kuwa usafirishaji wa mizigo kwa kutumia meli mbili zilizopo unakwenda kuchangamsha shughuli za kiuchumi katika Bandari ya Mbamba Bay .Pia watafanyabiashara watapaya fursa ya kusafirisha mizigo kwa gharama nafuu na mizigo itakuwa inafika kwa haraka zaidi.

Kuhusu kusimama kwa usafiri wa meli katika Bandari ya Mbamba Bay, Gallus amesema imechangia kukwamisha shughuli za kiuchumi kwani wapo ambao wameshindwa kusafirisha bidhaa zao ,hivyo Serikali ilona kuna mdororo huo na ndio maana imeweka nguvu katika usafiri wa meli ndani ya Ziwa Nyasa.

Amefafanua mel mara mwisho kufunga katika bandari hiyo ilikuwa mwaka 2017 na hivyo sasa huduma hizo zinakwenda kurejesha safari zake na hivyo kushauri wafanyabiashara na wananchi kutumia usafiri huo ambao ni nafuu na rahisi kuliko usafiri wowote na kusisitiza njia ya maji ndio inaweza kusafirisha mzigo mkubwa kwa muda mfupi zaidi.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Gomwanga Gems Ltd Iman Masawe ambao ni wadau wakuwa wa bandari ya Mbamba Bay kutoka na kusafirisha makaa ya mawe kwa kutumia usafiri wa meli katika Ziwa Nyasa amesema wanaipongeza Serikali kwa kuamua kuweka mkakati wa kuboresha miundombinu ya usafiri wa meli kwani utawawezesha kusafirisha makaa ya mawe kwa wateja wao kwa gharama nafuu tofauti na kutumia usafiri wa njia ya barabara ambao ni gharama kubwa.

"Kwetu sisi tunajisikia fahari kuona Serikali inavyoendelea kuboresha miundombinu ya bandari na meli katika Ziwa Nyasa, shughuli zetu za uchimbaji tunazifanya katika Wilaya ya Nyasa eneo la Mbamba Bay katika Kijiji cha Malini , hivyo bandari ambayo kwetu iko karibu na tutaitumia kikamilifu ni bandari ya Mbamba Bay, na tayari ujenzi wa barabara unaendelea na hivyo itakuwa rahisi kufika bandarini na kusafirisha makaa ya mawe ambayo tunayachimba katika mgodi wetu.

"Makaa ya mawe tunayochimba hapa kwetu ndio makaa ya mawe bora kuliko mengine yoyote katika mkoa wa Ruvuma na hivyo tumekuwa tukipata wateja wengi ambao wanahitaji kusafirishiwa na njia rahisi na gharama nafuu ni njia ya maji,"amesema Masawe na kuongeza katika eneo hilo kuna akiba ya kutosha ya makaa ya mawe na mkakati wao ni kuchimba tani 33000 kwa mwezi.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/39aOIBM
via
logoblog

Thanks for reading MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA YAANIKA MIPANGO YAKE YA KUIBORESHA BANDARI YA MBAMBA BAY

Previous
« Prev Post