Ticker

10/recent/ticker-posts

SMZ yaahidi kukamilisha sheria ya Diaspora kabla ya Mei 2020


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia hadhara ya Diaspora Tanzania (haipo pichani) katika kongamano la sita la diaspora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu, akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kuhutubia kongamano la sita la Diaspora  Mwenyekiti wa wanadiaspora, Bwn. Norman Jasson akitoa salamu za wanadiaspora wakati wa kongamano
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea moja ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo Zanzibar wakati alipotembelea banda la wajasiriamali, kabla ya kufungua rasmi kongamano la sita la Diaspora Tanzania. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akifuatiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene.
Baadhi ya ujumbe wa Diaspora ukiwa umesimama wakati wa kuimba wimbo wa taifa katika kongamano la sita la Diaspora lililofanyika Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein katikati (mwenye tai ya rangi ya blu bahari) akiwa katika picha ya pamoja na vinongozi waandamizi wa serikali pamoja na baadhi ya ujumbe wa Diaspora mara baada ya kufungua rasmi kongamano la sita la Diaspora Tanzania
Baadhi ya ujumbe wa Diaspora ukifuatilia hutuba ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kuhutubia kongamano la sita la Diaspora.
*******************************
Na Nelson Kessy, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, amewahakikishia wanadiaspora kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itasimamia na kuhakikisha kuwa sheria ya Diaspora inakamilika kabla ya mwezi Mei, 2020.

Rais Dkt. Shein ametoa kauli hiyo leo mjini Zanzibar wakati alipokuwa akifungua rasmi kongamano la sita la Diaspora ambalo limeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikianana Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-Zanzibar.

Dhamira ya kongamano hili kuendeleza ushirikiano uliopangwa na Diaspora na wawekezaji kama wadau wa maendeleo nchini chini ya kaulimbiu ya”mtu kwao ndio ngao”.

Ndugu wanadiaspora mwaka jana nilieleza jitihada za kuanziasha ofisi za Diaspora hapa Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati ule kwa kuanziasha Diaspora.

"Kutokana na kutambua umuhimu wa watanzania waishio nje ya nchi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliunda idara maalumu ya kushughulikia masuala ya Diaspora katika wizara ya Mambo ya nje mwaka2010 ili kuvitekeleza kwa vitendo azma yetu ya kuwashirikisha wanadiaspora Tanzania katika kuendeleza nchi yetu”.

Ameongeza kuwa kwa umuhimu huohuo, na kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 na kuyapa nguvu masuala ya Diaspora tulianzisha kitengo cha Diapora na baadae idara ya Diaspora ilinzishwa hapaZanzibar. Tulitengeneza sera maalumu ya wanadiaspora, na sasa tupo mbioni kuanzisha sheria ya Diaspora, nimefurahi kuwa rasimu ya sheria hiyo imefikia katika hatua nzuri.

”Kwa matiki hiyo basi, namuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Issa Haji Ussi Gavu kuhakikisha anasimamia kwa karibu sana utayarishaji na kukamilika kwa rasimu ya sheria hiyo na iwasilishwe kwenye Baraza la wawakilishikabla ya mwezi mei 2020,”. Amesema Dkt. Shein na kuongeza kuwa atahakikisha kuwa kabla ya kumaliza muda wangu wa Urais hapa Zanzibar sheria hiyo itakuwa imekaa vizuri kimkakati, kisera pamoja na kisheria kwaupande wa Zanzibar.

Aidha, Rais Shein, aliwapongeza wanadiaspora kwa michango yao ambayo wamekuwa wakiitoa kwa kusaidia Serikali, pamoja na mambo mengine michango hiyo imekuwa ikisaidia kijamiii na kiuchumi.

Awali akitoa salamu za wanadiaspora, Mwenyekiti wa wanadiaspora, Norman Jasson alisema kuwa mchakato wa sera ya Diaspora umekuwa ni wa muda mrefu na kumekuwepo na ukimya takribani miaka mitatu na kumuomba Rais Dkt. Shein kuwasaidia kusimamia zoezi hilo.

”Sera ya Diaspora ina umuhimu wa kipekee kwani tunaamini kuwa sera hiyo itakapokamilika itatoa majibu ya maswali mengi ambayo yamekuwa yakitunyima usingizi. Tunaamini sera hii itasaidia sio tu masuala ya uraiawan chi mbili au hadhi maalum, bali pia masuala mengine kama umiliki wa ardhi, mirathi, ndoa kwa wenyeji na wageni, ruhusa ya makazi nchini kupitia vibali au visa na mengine mengi” Amesema Bwn. Jasson.

Aliongeza kuwa, pia wanadiaspora wanaamini kuwa sera hiyo itarahisisha utungaji wa sheria itakayowatambua watanzania wote walio ughaibuni bila kujali kama tayari wameshachukua uraia wa nchi nyingine au kama tayariwana vibali vya makazi katika nchi wanazoishi na pia bila kujaliwaliingiaje ughaibuni katika kusaka maisha.

Bwana Jasson aliongeza kuwa, msingi wa wanadiaspora ni utanzania wao na utayari wa kushiriki katika jitihada za kusuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama vile kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini ambapokwa sasa TDC-Global tayari imewaleta Tanzania watu wenye nia ya kuwekeza.

”Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kushirikiana na Diaspora itafanikisha mambo mengi kwa kuanzisha mkakati wa wa kuhakikisha kuwa watanzania waishio nje ya nchi wanatayarishiwa mfumo ambao utasaidia kukusanya michango ya kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo”. Amesema Bwn. Jasson.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, George Simbachawene akitoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Shein amesema kuwa sera yaDiaspora kwa upande wa Tanzania rasimu ya kwanza tayari imekamilika na hatua inayofuata ni kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanadiaspora wenyewe kupitia balozi zetu ili na wao waweze kutoa mawazoyao.

”Mhe. Rais, kwa sasa sera ipo katika hatua nzuri, jitihada kubwa zinaendelea na jambo hili linahitaji kushughulikiwa kwa uangalifu mkubwa kwa sababu ya historia ya nchi yetu," Amesema Simbachawene.

Aidha, Waziri Simbachawene aliongeza kuwa ni muhimu kutumia wanadiaspora kama fursa, sekta muhimu katika ujenzi wa uchumi wa taifa letu na mataifa mengi dunini yanafanya hivyo.

Pamoja na mambo mengine, kongamano hili la sita la Diaspora limejadili mada saba ambazo ni urejeshaji wa taka za plastiki, Tanzania na uwekezaji, Diaspora na uwekezaji, Mradi wa nyumba za bei nafuu, kilimo cha kisasa, kubadili mfumo wa utalii wa Zanzibar pamoja na Mradi wa daraja la Zanzibar – Tanzania bara.

Mwezi Augusti, 2018 watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) walikutana Chake Chake, kisiwani Pemba katika kongamano la tano la Diaspora kufuatia utaratibu uliowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwakutanisha kila mwaka Watanzania waishio ughaibuni.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2PKPNHL
via

Post a Comment

0 Comments