Ticker

10/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI AWESO AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA MAJI MJI MDOGO MISUNGWI


Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akipita kukagua kazi ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Magu, mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (wa tatu kutoka kushoto) walipokuwa wakikagua Mradi wa Maji wa Magu, mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dkt. Philemon Sengati akitoa taarifa ya Sekta ya Maji ya wilaya kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakibadilishana mawazo wakitoka kukagua Mradi wa Maji wa Magu, mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na wananchi katika Mji Mdogo wa Misungwi, mkoani Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Leonard Msenyele akitoa maelezo kuhusu chanzo cha Mradi wa Maji wa Magu kwa Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akimsikiliza, mkoani Mwanza.

………………

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amevunja Bodi ya Mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo Misungwi (MIUWASA) kutokana na uendeshaji na usimamizi usioridhisha hali iliyosababisha huduma ya maji katika mji wa Misungwi kuzorota na kuwa kero kwa wananchi.

Akitangaza uamuzi huo, Aweso amesema amechukua maamuzi hayo baada ya kubaini mapungufu makubwa ya kiutendaji katika mamlaka hiyo na kujiridhisha kupitia taarifa iliyotokana na kikao alichokaa na viongozi wa Wilaya ya Misungwi.

“Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa Misungwi na uchunguzi uliofanyika tumegundua kuna tatizo kwenye mamlaka na uongozi wa wilaya umetuthibitishia baada ya kufanya mazungumzo’’, amesema Aweso.

“Kuanzia leo mji wa Misungwi utakuwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), lakini pia Mkaguzi wa Ndani kutoka wizarani atakuja kufanya ukaguzi wa hesabu za MIUWASA na kutupa taarifa yote ya mapato na matumizi yao’’, ameelekeza Aweso.

Awali, Naibu Waziri Aweso alisema wizara imetekeleza agizo la Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli kwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 623 kama malipo ya mkandarasi Kampuni ya Shanxi Construction Engineering Corporation ya China anayefanya kazi ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mbalika wilayani Misungwi chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Kahama-Shinyanga (KASHWASA).

Akisema na kiasi cha milioni 350 kimeshatolewa na milioni 273 iliyobaki itamaliziwa wiki ijayo, akifafanua kuwa fedha hizo ni ajili ya kukamilisha kazi zote zilizobaki na kuagiza mradi uwe umekamilika ifikapo Machi, 2020 kulingana na mkataba.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2LoUAgJ
via

Post a Comment

0 Comments