Ticker

10/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AFUATILIA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS

Kazi ya usafishaji wa barabara ya Mang’ombe – Iloganzala Km 1.2, inayojengwa kwa kiwango cha lami wilayani Mbogwe mkoani Geita ikiendelea ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli kuwataka TARURA kujenga barabara za lami zenye urefu wa km 3 wilayani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli wa kuwataka TARURA kujenga barabara za lami zenye urefu wa Km 3 wilayani Mbogwe.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Mbogwe mhe, Augustino Masele alipokagua utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli la kuutaka Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), wilayani Mbogwe kujenga kilometa 3 za barabara za lami katika makao makuu ya wilaya hiyo kulia ni mkuu wa wilaya hiyo Bi. Martha John Mkupasi.
Meneja wa (TARURA), wilayani Mbogwe mkoani Geita Eng. Justine Lukaga, akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua barabara ya Mang’ombe-Iloganzala Km 1.2, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umeanza katika mji wa Masumbwe Wilayani humo.
Muonekano wa barabara ya Mang’ombe-Iloganzala Km 1.2, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umeanza katika mji wa Masumbwe Wilayani Mbogwe Mkoani Geita.
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita Bi, Martha John Mkupasi (wapili kushoto), akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua barabara zinazojengwa na TARURA kwa kiwango cha lami wilayani humo.

………………….

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa amewataka viongozi wote wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kushirikiana na Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA), kuhakikisha ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Masumbwe unakamilika kwa wakati.

Amesema uwepo wa barabara nyingi za lami katika wilaya za Mbogwe na Kahama utachochea fursa nyingi za utalii, ufugaji, uchimbaji madini na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na hivyo kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na TARURA wilayani humo mhe. Kwandikwa amesema atahakikisha ujenzi wa kilomita zote tatu zilizoahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli unakamilika kama ilivyopangwa.

“Hakikisheni mnawaelimisha wananchi ili wapishe maeneo yote zitakapopita barabara hizo ili kusiwe na vikwazo kwa wajenzi wa barabara hizo”, amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.

Hivi karibuni katika ziara yake wilayani humo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli aliagiza utekelezwaji wa haraka wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa tatu alizoahidi katika makao makuu ya wilaya ya Mbogwe na kusisitiza kazi hiyo ifanyike haraka.

Naye mkuu wa wilaya ya Mbogwe Bi, Martha John Mkupasi amesisitiza umuhimu wa wananchi kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi wa barabara hizo na kuzilinda pindi zitakapokamilika ili kuboresha miundombinu ya wilaya hiyo na kukuza shughuli za biashara.

Amehimiza wananchi kutovamia maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuepuka usumbufu wakati zoezi la ujenzi linapoendelea.

Kwa upande wake meneja wa TARURA wilayani humo Eng. Justine Lukanga ameahidi ujenzi wa kilometa tatu za lami katika barabara ya Mashineni-Kasandalala km 1.3 na Mang’ombe-Iloganzala 1.2 na kituo cha afya-shuleni km 0.5 zitajengwa kwa kasi na ubora unaozingatia thamani ya fedha.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/365g7Tw
via

Post a Comment

0 Comments