Ticker

10/recent/ticker-posts

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WAAPISHWA RASMI

Na Woinde Shizza globu ya jamii,Arusha 

Jumla ya wasimamizi 30 wa Vituo vya kupiga kura wameapishwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha mapema jana Novemba 21, 2019 na Hakimu Mkazi  Itikija Theoflo Nguvava .
Akizungumza na wasimamizi hao baada ya kuapishwa Msena Bina ambae ni msimamizi wa uchanguzi Wilaya ya Arusha amesema ni muhimu wasimamizi kuzingatia  kiapo hicho cha utii, uadilifu na uaminifu kwani  ndicho kitakacho waongoza katika kuwasimamia wapigakura ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wapiga kura ni Raia wa Tanzania, asiye na umri chini ya miaka 18, Mkazi wa Mtaa husika, aliye jiandikisha katika daftari la wapiga kura na awe anaakili timamu.
Hata hivyo Msena amesema mpiga kura awe na kitambulisho chochote kitakacho mtambulisha chenye picha yake mfano kitambulisho cha Utaifa, cha mpiga kura, Bima ya afya, Leseni ya udereva  na Pasi ya kusafiria .
Pamoja na hayo wasimamizi  wamehimizwa kuzingati muda wa kufungua na kufunga vituo ambapo ni saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 10:00 Jioni na kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu, wazee, wamama wajawazito na wanaonyonyesha.
“Tume waamini ndio maana tumewateua  hivyo mzingatie viapo vyenu  mkafanye kazi kwa uadilifu, uaminifu na utii pia katika kipindi hiki epukeni kutumia vilevi”  alisema Msena Bina.
Alitumia muda huo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wao bora watakao watakao weza kuwaongoza na kuwaletea maendeleo katika vijiji vyao ,huku akiongeza kuwa kupiga kura ni haki yao ya msingi hivyo wasikubali ipotee bila kushiriki.
Mmoja wawasimamizi hao ambaye akutaka jina lake gazetini alisema kuwa wamepokea maelekezo yote na watafanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni zote zilizowekwa.
Wasimamizi 30 wa Vituo vya kupiga kura wakiapishwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha mapema jana Novemba 21, 2019 na Hakimu Mkazi Itikija Theoflo Nguvava .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2OazcNS
via

Post a Comment

0 Comments