RAIS MAGUFULI AMPA MAAGIZO MAZITO CAG MPYA,AMWAMBIA AKACHAPE KAZI

  Masama Blog      
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ambao ni  Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu  za serikali, Katibu Tawala, Balozi, Kamishna wa kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu, na Majaji 12 wa mahakama kuu pamoja na Mwenyekiti, na makamu mwenyekiti na  Makamishna watano wa Tume ya Haki za binadamu na utawala bora.

Akizungumza na viongozi hao wateule, Rais Magufuli amesema kuwa walioteuliwa wasidhani kuwa hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, Pia amewashauri majaji wakafanye kazi kwa haki bila kumuonea Mtu, kwani hukumu hutolewa na Mungu tu, ila kwa hapa duniani tunao Majaji. 

"Kuna watu ukiwateua wanadhani hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, wewe (CAG) nilipokutoa toka kuwa Mkurugenzi wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) kwenda kuwa Katibu Tawala mkoa hukusema neno na ulikuwa mtulivu ,wapo wengine ukiwatoa wanasema maneno maneno, wakati huo unapowateua huwa hawasemi" Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemuasa Mkaguzi Mkuu wa  Hesabu za Serikali kutokuwaonea watu pale anapopewa maagizo na mihimili  mingine kama Bunge na Mahakama, akatekeleze majukumu yake kwani yeye ni mtumishi na asibishane.

"Najua CAG una 'Qualification' nzuri tu na huwa hatufanyi makosa tunapoteua, form four ulitoka na divison one, form six ukatoka na division one hii ni kuonesha wewe ni kipanga sio kilaza, 'Degree'  ya sheria unayo, ukachukua na masters, umefanya kazi sehemu nyingi tu" Amesema Rais Magufuli.
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo Novemba 4,2019 amemuapisha  Charles  Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana. Hafla ya kumuapisha Kichere ambaye kabla ya  uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe pamoja na viongozi wengine, imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2WFqmtZ
via
logoblog

Thanks for reading RAIS MAGUFULI AMPA MAAGIZO MAZITO CAG MPYA,AMWAMBIA AKACHAPE KAZI

Previous
« Prev Post