Ticker

10/recent/ticker-posts

DC CHONGOLO AWAWEKA NDANI WAKANDARASI WA KAMPUNI YA CRJE KWA KUSHINDWA KUKAMILISHA MRADI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA KWA WAKATI.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo amewashikilia wakandarasi wawili wenye asili ya china wa Kampuni ya CRJE kwa kushindwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande.

Mhe. Chongolo amefikia uamuzi huo leo mara baada ya kampuni hiyo kushindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati huku Mhandisi mshauri wa Manispaa Emanuel Tilya akisisitiza kuwa wamekuwa hawatoi ushirikiano wowote licha ya kwamba yupo kwenye eneo la mradi.

Akizungumza wakati wa ziara aliyoifanya leo ya kukagua miradi inayojengwa na Halmashauri hiyo, Mhe. Chongolo amefafanua kuwa kwa muda mrefu amekuwa akizungumza na mkandarasi huyo kuhusu kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa lakini hawakufanya hivyo.

Ameeleza kuwa halmashauri inahitaji kiwanda hicho haraka ili kiweze kutumiwa na wananchi ambao ndio wanufaika wa mradi huo lakini mkandarasi aliyepewa kazi hiyo anawarudisha nyuma.

Ameeleza kuwa halmashauri imeshawalipa fedha kwa ajili ya ujenzi huo lakini kinachofanyika ni fedha hizo kuzipeleka kwenye miradi yao mingine jambo ambalo limefanya hadi sasa kusuasua kwa mradi.

“ Nimekuja hapa zaidi ya mara tatu, mara ya kwanza nilikuja nikaongea nao wakaniahidi watakamilisha kwa muda uliopangwa, mara ya pili nilikuja hapa nikafoka hadi nikakasirika lakini hali imeendelea hivi hivi, sasa sijawakamata nimewashikilia hadi pale watakapoleta mpango kazi wao uliojitosheleza.“ amesema Mhe. Chongolo.

”Hatuwezi kukaa na watu wa namna hii, tumetoa pesa nyingi, kwa ajili ya kukamilisha mradi huu mapema halafu wanatuchezea, ,kama wakileta leo, kesho nitawaachia, kadiri watakavyowahi kuniletea huo mpango kazi wao ndio na mimi nitawaachia, Askari kamata hao waweke ndani.

Askari huyo wa kituo cha polisi Mabwepande alitii agizo hilo na kuwapakiza kwenye gari kuelekea kituoni huku Mhe. Chongolo akiwafuata nyuma ili kuhakikisha kuwa wamefikishwa mahali husika.

Mhe. Chongolo alisisitiza kuwa hajaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa kiwanda hicho na kuagiza wasiachiwe hadi atakapotoa agizo ikiwa ni baada ya kutekeleza walichoambiwa.

Awali Mhandisi mshauri wa Manispaa, mhandisi Tilya ,amesema kuwa walikubaliana kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati lakini kilichotokea ni tofauti huku mafundi wanne tu ndio waliokuwa wanafika eneo hilo la mradi.

Alifafanua kuwa “ wakati mwingine huwa tunagombana wenyewe kwa wenyewe, kama angekuwa na uwezo wakufanya kazi kama msambazaji wake ingekuwa sawa, kwani anauwezo wakubeba kiubiki mita. 150 hadi kufikia saa 8.00 mchana, inamana tukifanya kazi usiku na mchana tunaweza kufikia kiubiki mita .300 kwa siku.

Alifafanua kuwa eneo la kiwanda hicho kinaukubwa wa mita zaidi ya 4070 ambapo hadi sasa tayari imeshafanyika kiubiki mita 491 sawa na asilimia 12 na kwamba iliaweze kufanikisha hanabudi ndani ya mwezi mmoja kwa usiku na mchana jambo ambalo alisema mkandarasi huyo hawezi kufanya.

Mhandisi huyo alifika mbali zaidi nakusema kuwa “ hakuna ushirikiano ambao anapata kutoka kwao , wanachoendelea kukifanya hapa ni kukudanganya mkuu. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo akiwa sambamba na wakandarasi wa kampuni ya CRJE katika eneo la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa Mabwepande alipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya ujenzi wake.
 Eneo la juu la ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa ndani ya Manispaa ya Kinondoni katika kata ya Mabwepande.
 Mafundi wakiendelea na kazi katika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa Kata ya   Mabwepande katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo akiwa sambamba na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Samweli Lyiza wakati wakikagua mradi wa kiwanda cha kuchakata taka kinachojengwa katika Kata ya Mabwepande



from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35hrXJK
via

Post a Comment

0 Comments