Ticker

10/recent/ticker-posts

Tanzania yagundua gesi zaidi katika sehemu nne tofauti -


Bomba la mafutaHaki miliki ya pichaAFP
Serikali ya Tanzania imegundua maeneo manne tofauti ambayo yana uwezo mkubwa wa kupatikana kwa gesi asli na sasa imetoa wito kwa wawekezaji kufanya utafiti zaidi.
Waziri wa kawi Medard Kalemani aliambia mkutano wa mafuta na gesi 2019 kwamba maeneo hayo ni pamoja na Ntoria, Magharibi mwa Songosongo , Mnazi bay kaskazini na Ravu kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
''Maeneo hayo yana uwezo mkubwa wa kutoa futi trilioni 5.2 zenye ujazo mraba baada ya kuchimba'', alisema.
Kulingana na Gazeti hilo amesema kwamba Ravu pekee ina uwezo wa kutoka futi trilioni 2 mraba katika ujazo , magharibi mwa Songosongo futi trilioni 1.3 zenye ujazo mraba na kaskazni mwa Mnazi Bay futi trilioni 0.3 mraba.
Iwapo ugunduzi huo utathibitishwa , utimarisha kiwango cha gesi iliogunduliwa nchini humo kutoka futi trilioni 57.5 zenye ujazo mraba mraba hadi futi trilioni 62.7 zenye ujazo mraba.
Uwekezaji huo sio wa kutafuta na kuchimba visima vipya pekee bali pia katika gesi iliopo tayari.
Tunataka wawekezaji zaidi katika sekta kuongeza matumizi kwa kuwa utumizi uko chini sana, alisema.
Kulingana na waziri huyo ni asilimia moja pekee ya gesi asli iliogunduliwa iliotumika katika kipindi miaka 15 iliopita.
Wito huo kwa wawekezaji unajiri wakati ambapo serikali inaangazia upya sheria ya uwekezaji ya 1977, huku muswada ukitarajiwa kusomwa bungeni mwezi wa Novemba.
Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri katia wizara ya waziri mkuu Angellah Kairuki walisema kwamba ofisi yake tayari imeandika muswada huo unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni mwezi ujao kwa mjadala.
''Siwezi kusema kilichopo ndani ya muswada huo lakini unalenga kuweka mazingira mazuri na kuwavutia wawekezaji na biashara'', alinukuliwa na The Citizen tanzani akisema.
Kulingana na yeye serikali kwa sasa inaangazia sera ya uwekezaji iliopo ili kuhaikisha kuwa zinaambatana na sheria mpya ya uwekezaji.

Gesi zaidi yagunduliwa pwani ya Tanzania

Bomba la mafutaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwaka 2016, Tanzania iligundua takribani futi za ujazo trillioni 2.17 za Gesi katika eneo la Ruvu lililoko katika Mkoa wa Pwani kilomita chache kutoka mji mkuu wa biashara-Dar es Salaam.
Huu ulikuwa ugunduzi mkubwa zaidi wa gesi pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi.
Kwa mujibu wa Badra Masoud, aliyekuwa msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania, ugunduzi huo ulikuwa na thamani ya takribani shilingi za Tanzania trillioni 12 sawa na takribani dola za Kimarekani bilioni 6.
Tanzania bado inaamini huenda kuna gesi zaidi itagundulika kwa kuwa utafiti zaidi bado unaendelea.
Msemaji huyo wa Wizara ya Nishati alisema kuwa utafiti kuhusu Gesi hiyo umedumu kwa takribani miaka hamsini ukihusisha makampuni mbalimbali.

Gesi yaanza kutumika Tanzania

Mwaka 2015, Shirika la maendeleo ya Petrol nchini Tanzania lilisema kuwa Mradi wa Gesi iliyogunduliwa kusini mwa nchi hiyo ,mkoani Mtwara umefikia asilimia 94 na tayari gesi hiyo imeanza kutumika katika baadhi ya maeneo.
Kufiuka wakati huo baadhi ya viwanda, na mashirika yalikuwa yameanza kutumia gesi hiyo asilia hatua inayodaiwa kupunguza gharama za upatikanaji wa Nishati kwa baadhi ya wakazi ambao wamekuwa wakitumia gharama kubwa ili kupata Nishati .


from CCM Blog https://ift.tt/2o7u6b8
via

Post a Comment

0 Comments