Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 05.10.2019: Griezmann, Neymar, Maddison, Mandzukic, Willian, Odegaard,

  Masama Blog      


Antoine GriezmannHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAntoine Griezmann
Barcelona huenda ikamjumuisha mshambulizi wa kimataifa wa Ufaransa wa miaka 28, Antoine Griezmann katika mkataba wa kumsajili tena mshambuliaji nyota wa Brazil Neymar, 27, kutoka Paris Saint-Germain msimu ujao. (Le10Sport - in French)
Chelsea inamatumaini kuwa mlinzi wake Fikayo Tomori, 21, na mshambuliaji Tammy Abraham, 22, watasaini mkataba mpya wiki chache zijazo.
Wachezaji hao wawili wamejumuishwa katika kikosi England cha kufuzu kwa kintang'anyuro cha Euro 2020 baadae mwezi huu. (Standard)
Chelsea pia inakaribia kufanya mazungumzo ya wazi ya mkataba na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil wa miaka 31- Willian, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika mwisho wa msimu huu. (Express)
WillianHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMshambuliaji wa Kimataifa wa Brazil, Willian
Manchester City haina mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Norway aliye na umri wa miaka 20 Martin Odegaard, ambaye yuko Real Sociedad kwa mkopo kugoka Real Madrid. (Manchester Evening News)
Kocha wa Everton Marco Silva amesema mchezaji wa safu ya mashambulizi ya England ya wachezaji wa chini ya miaka-19 -Anthony Gordon, 18, anakaribia kujiunga na kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Liverpool Echo)
Marco SilvaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKocha wa Everton Marco Silva
Manchester United inafuatilia kwa karibu mchezo wa mshambuliaji wa Klabu ya Leon wa miaka 20 Mmexico Jose Juan Macias, ambaye amebatizwa jina la 'Javier Hernandez wa baadae'. (Marca via Express)
West Ham inamnyatia kiungo wa kati wa miaka 20 raia wa Bolivia, Daniel Camacho, ambaye anachezea klabu ya nyumbani ya Aurora. (Diez via Sport Witness)
Real Madrid inapania kumuajiri meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte kama kocha wao mpya baada ya kumfuta kazi Julen LuLutetiu mwaka jana lakini uamuzi huo ukabatilishwa kufuatia ushauri wa nahodha Sergio Ramos.(Fichajes.net via Mail)
Sergio Ramos
Image captionnahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos
Manchester United inamsaka mshambuliaji wa Urusi wa miaka 20 Aleksandr Sobolev, nayechezea klabu ya PFC Krylia Sovetov Samara inayoshiriki Ligi Kuu ya Urusi. (Mirror)
Kocha wa Anderlecht, Vincent Kompany anamlenga mlinzi wa Wales Ashley Williams,35, mkataba wake na Bristol City utakapokamilika mwezi Januari. (Sun)
Kiongo wa safu ya mashambulizi ya Croatia, Mario Mandzukic, 33, anayelengwa na Manchester United nu miongoni mwa wachezaji watatu watakaouzwa na Juventus mwezi January. (Calciomercato - in Italian)
Mario MandzukicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMario Mandzukic miongoni mwa wachezaji watakaouzwa na Juventus msimu ujao
Mlinzi wa zamani wa Tottenham na Arsenal Sol Campbell na mshambuliaji wa zamani wa Celtic na Barcelona Henrik Larsson wamehojiwa kuchukua wadhifa wa meneja wa Southend. (Sky Sports)
Stakabadhi iliyovujishwa umefichua kiwango cha faini Real Madrid inayowatoza Inawatoza wachezaji wake kwa kukiuka sheria kama vile kuchelewa kufika kwa mazoezi nakutumia simu wakiwa katika basi la timu au chumba cha kubadilisha mavazi. (Marca)

Tetesi Bora Ijumaa

Kocha wa zamani wa England Fabio Capello amefichua kuwa alijaribu kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi kwa mkopo kipindi akiinoa timu ya Juventus. (Sky Sports Italia via Mail)
Lionel MessiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kocha wa Arsenal Unai Emery amegoma kukanusha uwezekano wa kiungo Mesut Ozil kuihama klabu hiyo mwezi Januari. (Sun)
Kiungo nyota wa Tottenham Christian Eriksen bado anaamini mipango yake ya kuhamia Real Madrid inaweza kufanikiwa, na wakala wake mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kwenda Uhispania kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Madrid. (Star)
Christian EriksenHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiungo nyota wa Tottenham Christian Eriksen
Mchezaji wa Callum Wilson, 27, wa Bournemouth yupo katika rada ya usajili wa klabu ya Manchester United ambao wanatafuta kwa nguvu zote mshambuliaji wa kusajili katika dirisha dogo la mwezi Januari. (Sky Sports)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski ametoa kauli ya kebehi kwa wapinzani wake wa zamani Tottenham kwa kusema kuwa Serge Gnabry inabidi awe mchezaji bora wa mwezi wa Arsenal.
Gnabry ambaye amewahi kuichea Arsenal alifunga goli nne peke yake wakaqti Bayern ikiidondoshea Spurs goli 7-2 wiki hii.


from CCM Blog https://ift.tt/2LMZ693
via
logoblog

Thanks for reading Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 05.10.2019: Griezmann, Neymar, Maddison, Mandzukic, Willian, Odegaard,

Previous
« Prev Post