Ticker

10/recent/ticker-posts

HAKIKISHENI KILA KAYA INAKUWA NA UMEME HADI IFIKAPO NOVEMA 16-KALEMANI

Na Woinde shizza, Simanjiro

Waziri wa  Nishati  Dkt Medard Kalemani  amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi, mameneja wa tanesco   kuwahamasisha wananchi waliopo katika Wilaya zao kulipia umeme ili waweze kuvutiwa umeme katika kaya zote. 

Aidha alimtaka Mkandarasi ambaye ni Angelique International Ltd kwa kushirikiana na shirika la Umeme Tanesco wilaya ya Simanjiro na mkoa wa Manyara kwa ujumla kuhakikisha wananchi wote wilaya ya Simanjiro katika vijiji vyote pamoja na vitongoji vyote vinapata umeme na sio mradi Umeme tu bali ni Umeme wa uhakika. 

Aliyasema hayo jana wakati akiongea na wananchi  wa Kijiji cha  Naepo kilichopo katika kata ya Naisinyai wilayani simanjiro mkoani Manyara ambapo mbali nakuongea na wananchi hao pia alizindua mradi na kuwasha Umeme katika Shule ya msingi Naepo pamoja na shule ya sekondari ya Shambarai zote zipo katika Wilaya hiyo. 

Kalemani alisema kuwa anafahamu katika kijiji cha naisinyai kimeshapata Umeme lakini haujatosheleza, lakini pia katika vijiji vingine pia vimepata umeme ,ambapo alibainisha kuwa anafatilia katika vijiji vyote ambapo avina umeme vinapata Umeme 

"napenda kutoa maelekezo kwa Mkandarasi pamoja na Tanesco wilaya ya simanjiro hadi ikifika November 16 vijiji vyote pamoja na kaya zote za Kata ya Naisinyai viwe vimepatiwa Umeme ,namaanisha kitongoji cha naepo kiwekimejaa Umeme ,kambi ya chokaa kulipelekwa Umeme lakini bado ujaja sasa napenda kukwambia Mkandarasi kabla ujatoka hapa hakikisha kaya zote, vijiji vyete pamoja na kitongoji cha kibaoni kiwe kimejaa Umeme  zinaumeme"alisema Kalemani 

Aliwataka Wananchi kujitokeza kwa kasi sawa ya muheshimiwa Rais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania John Magufuli kuunganisha Umeme katika nyumba zao ,alibainisha kuwa Umeme huu hautaruka Nyumba ,kitongoji, kijiji na hata kaya  na wajibu wao wananchi ni kulipia tu kiasi cha shilingi elfu 27000 na kuunganishiwa Umeme. 

"napenda kuwaambia wananchi kama nyumba yako niyamakuti ,ni tembe ama ni yaudongo au ya gorofa zote zinastaili kuwekewewa umeme ,hakuna nyumba isiofaa kuwekewe Umeme na olewake Mkandarasi au muhandisi au Meneja aruke nyumba eti kwasababu ni mbaya ,hoho utakuwa wewe ni mbaya nanapenda kukuhakikisha autabaki salama "alisema  Kalemani 

Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Naepo Kaika  Mevukori aliishukuru serikali kwa kuwaletea umeme katika Kijiji chao Kwani umeme uwo utawasaidia kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo Kufunga mashine za kusaga na kukoboa, Kupungua maduka ya kuuza vifaa vya umeme pamoja na kuendeleza shughuli mbalimbali ambazo Zilikuwa zikitegemea Umeme. 

Naye  Lazaro Charles alisema wakati hakuna Umeme walikuwa wanatembea kilimeta kumi na mbili kwenda kufata huduma za umeme kama vile kuchaji simu ,pia walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda kusaga mahindi kwa ajili ya chakula ,aidha pia alisema pia Umeme huu uliowashwa katika shule hizi utawawezesha wanafunzi kupata muda wa ziada wa kujisomea na  hata Waalimu kupata muda wakuandaa Vipindi namitiani kwaajili ya mwanafunzi 

Kwa upande wake Laitiness Lowasa Sainyei aliomba serikali iongeze kasi zaidi ya kusambaza umeme ili vijiji ambavyo avina viweze kupata na wananchi waweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo zinategemea umeme

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco wilaya ya Simanjiro, Zakaria Masatu aliishukuru serikali kupitia Wizara ya Nishati Kwa kuendelea kuwa karibu na Shirika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali na hivyo kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya wananchi wa wilaya ya simanjiro na Tanzania kwa ujumla 

Alisema kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali iliwemo udogo wa wigo wa mradi kulinganisha na mahitaji ya wananchi, pia alibainisha kuwa changamoto ingine inayolikabili  shirika hilo wilaya ya simanjiro ni pamoja na hujuma katika miundo mbinu hasa kuibiwa nyaya za copper kwenye transfoma na baadhi ya Watu wasio waadilifu. 

Alibanisha kuwa wao kama shirika wanaendelea kumsimamia Mkandarasi ili kuhakikisha anajenga miundombinu yenye ubora pia akamilishe Kazi katika muda uliopangwa.
Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na Wananchi Wakijiji cha Naepo kilichopo katika Kata ya Naisinyai jana mara baada ya kuzindua mradi wa umeme na kuwasha umeme katika Shule ya msingi ya Naepo iliopo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara (picha na Woinde shizza, Manyara) 
Meneja wa Tanesco wilaya ya Simanjiro Zakaria Masatu akiongea mbele ya Waziri wa nishati
Waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na Wananchi Wakijiji cha Naepo kilichopo katika Kata ya Naisinyai jana mara baada ya kuzindua mradi wa umeme na kuwasha umeme katika Shule ya msingi ya Naepo iliopo katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara (picha na Woinde shizza, Manyara) .


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/35JKJdE
via

Post a Comment

0 Comments