KIWANDA CHA TANICA CHAZIDI KUPAA KULELENI

  Masama Blog      
 Meneja Mkuu wa kiwanda cha TANICA, Linus Leopord  kilichoko mkoani Kagera
Kiwanda cha kahawa TANICA kilichoko mkoani Kagera


Na  Eben-Ezery   Mende
KIWANDA cha Tanganyika Instant Cofee Co. Ltd (TANICA) kilichohujumiwa na kusababisha kubadilishwa uongozi wa kiwanda hicho sasa kiko kwenye hatua za mafanikio kwa asilia 89.

Akizungumza na   Michuzi Blog,  Meneja Mkuu wa TANICA, Linus Leopord alisema waliokihujumu kiwanda hicho na kusababisha kufukuzwa kazi wanatapatapa kukichafua kiwanda hicho lakini hawawezi kwani mafanikio ya uzazishaji yanapanda kila siku.

Leopord alisema kiwanda hicho kilichoko mkoani, Kagera kinachozalisha kahawa ya unga (instant coffee) na kahawa ya kukaanga (roasted coffee) tangu mwaka 2012 hadi 2017 kilikuwa kikiendeshwa kwa kutengeneza hasara ya wastani wa sh. milioni 576 kwa mwaka.

Aidha alibaibisha kuwa baada ya kufanyika uchunguzi na viongozi waliohusika kusababisha hasara hiyo kufukuzwa kazi kumekuwepo vurugu na hujuma mbalimbali za kutaka kiwanda hicho kiporomoke lakini jitihada hizo zimegonga mwamba.

Alisema kiwanda hicho kwa msimu wa 2018/2019 kimepata mapato ya sh. bilioni 7.6 ambayo ni asilimia 85 ya bajeti ya kampuni hiyo kwa mwaka.

Kwa mujibubwa, Leopord TANICA inampango wa kutoa gawio kwa faida iliyopatikana ambayo ni sh. milioni 330 ikilinganishwa na faida iliyopatikana mara ya mwisho mwaka 2012 ya sh. milioni 10.

Alisema menejimenti ya awali iliyokuwa inakihujumu kiwanda hicho ilisababisha hasara ya deni la sh bilioni 3 ambapo hadi sasa TANICA imeshalipunguza deni hilo na kubaki sh bilioni 1.4.

Hata hivyo, Leopord alisema viongozi waliofukuzwa kazi kutokana na hujuma hizo wamekuwa wakisababisha atumie muda mwingi kujibu malalamiko yao ikiwemo mashauri mahakamani badala ya kuutumia muda huo kuendeleza mipango ya maendeleo ya kiwanda.

Alisema TANICA inampango wa kuongeza kipato chake kutoka sh bilioni 3-5 cha awali na kufikia sh bilioni 13 kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.

TANICA ni kampuni binafsi iliyosajiliwa chini ya sheria ya kampuni mwaka 1963 na kuanza uzalishaji rasmi mwaka 1967 baada ya kuzinduliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Soko kuu la bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda cha TANICA liko, Uganda, Dubai, China na Uholanzi.

Wamiliki wa kiwanda hicho ni Serikali/hazina, vyama vya ushirika ikiwemo Kagera cooperative union, (KCU) Karagwe District Cooperative union (KDCU) na Shirikisho la vyama vya Ushirika (TFC).


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/32ENgnn
via
logoblog

Thanks for reading KIWANDA CHA TANICA CHAZIDI KUPAA KULELENI

Previous
« Prev Post