MCHUNGAJI NA WAKE ZAKE WAWILI WAHUKUMIWA LEO JIJINI DAR

  Masama Blog      
Mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33), akiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kabla ya kusomewa humumy ya kwenda jela mwaka mmoja ama kulimba faini ya shilingi milioni moja.
Wake wa mchungaji wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33) wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo.

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
MCHUNGAJI  wa Kanisa la The Early Church of Lord Yeshwah, David Chirhuza (33), wake zake wawili na mdogo wake, wamehukumiwa kulipa faini ya ya jumla ya Sh. Milioni tano ama kwenda jela miaka miwili baada ya kukiri kosa la kuingia nchini na kufanya kazi ya kichungaji bila ya kuwa na kubali cha makazi. 

Hukumu hiyo imesomwa leo Septemba 10, 2019 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando baada ya washtakiwa wenyewe kukiri makosa na kuongeza kuwa baada ya washtakiwa hao kulipa faini au kutumikia kifungo hicho watuhumiwa hao ambao ni raia wa Kongo wanatatakiwa kurudishwa nchini kwao.

Akifafanua adhabu hiyo, Hakimu Mmbando amesema, katika shtaka la  kwanza washtakiwa wote kwa pamoja wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni moja au kwenda jela mwaka mmoja kila mmoja na katika shtaka la pili linalomuhusu mchungaji peke yake amehukumiwa kulipa faini ya  Sh. milioni moja au kwenda jela mwaka mmoja.

Kwa maana hiyo,  mchungaji  peke yake anahukumiwa kulipa faini ya Sh, milioni mbili ama kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani.
Washtakiwa wengine ni wake wa Mchungaji ni Esther Sebuyange (27), Kendewa Ruth (26) na Mshtakiwa mwingine mdogo wa Mchungaji, Samuel Samy (22).

Mapema, wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji Godfrey Ngwijo  akisaidiana na Sitta Shija, waliwakumbushia washtakiwa mashtaka yao na walidai kwamba, Septemba 2 mwaka huu eneo la Salasala Kilimahewa, Dar es Salaam, mchungaji huyo na wenzake walibainika kuingia nchini bila kibali.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa mchungaji huyo pekee alibainika  kujihusisha na kazi za kanisa akiwa hana kibali cha makazi.

 Hata hivyo, kabla ya kusomewa adhabu yao washtakiwa wote waliomba mahakama iwasamehe, isiwape adhabu kali, Mchungaji amesema kazi alivyokuwa akiifanya ya kuhudumia jamii si biashara pia kusimamia sheria.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/32zBDOs
via
logoblog

Thanks for reading MCHUNGAJI NA WAKE ZAKE WAWILI WAHUKUMIWA LEO JIJINI DAR

Previous
« Prev Post