WAKUU WA NCHI SADC WAIPITISHA LUGHA YA KISWAHILI KUANZA KUTUMIKA RASMI...RAIS MAGUFULI AWASHUKURU

  Masama Blog      
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAKUU wa Nchi na Viongozi wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)wamepitisha kwa kauli moja lugha ya kuwa lugha rasmi ya nne itakayotumika kwenye jumuiya hiyo.

Kupitishwa kwa lugha hiyo kumetokana na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais Dk.John Magufuli kuomba lugha hiyo iingizwe kwenye jumuiya hiyo.

Akizungumza leo Agosti 18,2019 kwenye ufungaji wa Mkutano Mkuu wa 39 wa SADC ambao umefanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere Mwenyekiti huyo mpya ametoa taarifa ya kupitishwa kwa lugha ya Kiswahili kuwa rasmi.

"Nianze kutoa hotuba yangu ya kufunga mkutano wa 39 wa SADC kwa kueleza hapa,nilitoa ombi kuhusu lugha ya Kiswahili kutumika kwenye SADC.Wakuu wanachama wameiteua
lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya  nne ya SADC.

"Narudia tena nawashukuru wakuu wa nchi na wakuu wa Serikali kwa kukubali lugha hiyo iwe rasmi kwenye jumuiya yetu.Baba wa Taifa amekuwa na heshima kubwa sana katika Bara la Afrika.Katika maisha wapo wanajitolea kwa mambo mbalimbali, wapo wanatoa figo,wapo wanaotoa fedha na utoaji wa aina nyingine," amesema.

Amefafanua Mwalim Julius Nyerere yeye aliamua kutoa upendo na maisha yake kwa ajili ya wengine na hivyo sehemu kubwa ya maisha aliyatumia kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa salama  na ndio maana nchini Tanzania kuna maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa kambi za wapigania uhuru na hasa nchi za Kusini mwa Afrika.

" Mwalimu Nyerere alishiriki kwa vitendo kwa ajili ya kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa huru.Tanzania imekuwa na kambi nyingi za wapigania uhuru na mojawapo ilikuwa eneo la Kongwa ambako anatoka  Spika wa Bunge Job Ndugai.

"Namshukuru Rais wa Afrika Kusini kwani ametemblea eneo la Mazimbo mkoani Morogoro ambako kuna makaburi ya mashujaa wa Afrika Kusini.Rais wa Afrika Kusini alikutana na mabinti wawili ambao walikuwa wanamtafuta baba yao,

"Na majina yao yameonekana katika makaburi hayo.Ni uchungu sana lakini kwa sehemu kubwa inaonesha  ni namna gani Mwalimu Nyerere aliwapenda wengine," amesema Rais Magufuli.

Amefafanua kwamba wote ambao walikuwa kwenye harakati za kupigania uhuru walikuwa wanatumia lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuwasaliana.Hivyo ameshukuru lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi ya nne kwenye jumuiya yetu.Mmemfuta machaozi baba wa Taifa.

"Kwa niaba ya Watanzania tunashukuru sana kwa lugha hii kuwa rasmi.Hivyo uamuzi huu wa kuifanya lugha hii kuwa rasmi itainganisha wananchi wetu.Kwa nchi ambazo hawazungumzi Kiswahili, Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kutoa walimu wa somo la Kiswahili kwa ajili ya kuwafundisha wananchi wao," amesema.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Z63Mug
via
logoblog

Thanks for reading WAKUU WA NCHI SADC WAIPITISHA LUGHA YA KISWAHILI KUANZA KUTUMIKA RASMI...RAIS MAGUFULI AWASHUKURU

Previous
« Prev Post