TCRA yawaomba mabalozi kutafuta wawekezaji Viwanda vya kuunganisha simu Janja

  Masama Blog      
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imewaomba mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali za nje kutafuta wawekezaji watakaoweza kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha simu janja maarufu Smartphone hapa nchini.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba mara baada ya kumaliza kwa ziara ya mabalozi 43 wa Tanzania nje ya nchi walioifanya katika mamlaka hiyo.

Amesema nchi bado inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa simu janja katika maeneo mbalimbali hasa vijijini hivyo fursa ambayo kwa sasa ipo nchini ni kuwa na kiwanda cha kuunganisha simu hizo ili ziweze kupatikana kwa wingi.

“Kutokana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa simu janja maarufu Smartphone tumewaomba mabalozi wetu watusaidie kuwatafuta wawekezaji watakowekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha simu hizo hapa nchini,” amesema.

Kilaba amesema mbali na hilo pia ameomba kutafutwa kwa wawekezaji watakaowekeza katika kiwanda kitakachotengeneza simu ambazo zimeharibika au kumaliza muda wake wa matumizi.

“Tuna simu zaidi ya milioni 40 zinazotumika kwa sasa na zipo majumbani mwa watu, lakini tukijuliza tangu tuanze sekta ya mawasiliano ni simu ngapi ambazo hazitumiki watu wameziweka tu, hivyo uwepo wa kiwanda utasaidia hizi kuchukuliwa kwani madini mbalimbali kama dhahabu, shaba yaliyopo kwenye simu yanaweza kuchambuliwa na kupata rasilimali, ila mabaki yakisagwa yatatengeneza kitu kingine,” alisema Kilaba. 

Aidha amesema lengo la ziara ya mabalozi hao ni kuangalia sekta ya mawasiliano inakabiliwa na changamoto na fursa gani ambazo zipo kwa ajili ya wao kwenda kutafutia ufumbuzi maeneo ambayo wanafanyia kazi.


Naye Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Naimi Aziz amesema kuwa wameamua kuja TCRA ili kuweza kujionea kwa macho yao wenyewe jinsi mawasiliano yanavyofanyika hapa nchini.

Amesema yeye na mabalozi wenzake wamefarijika kupata maelezo mazuri na ya kiutalaamu kuhusu shughuli mbalimbali ikiwamo miamala ya simu pamoja na undeshwaji wa mitambo inayofanywa na mamlaka hiyo.

“Tumeweza kufahamu kwa siku ni mawasiliano ya namna gani ambayo yanafanyika hapa nchini kwetu hasa yale yanayoingia na kutoka, tumefarijika kuona kwamba wataalum waliopo TCRA ni watanzania,” alisema Aziz.


Amesema pia wametambua changamoto mbalimbali zinazoikabili TCRA ikiwamo masuala ya mitambo pamoja na wawekezaji na wao kama mabalozi watajipanga namna ya kuweza kuwasaidia kuzitatua.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk. Abadllah Possi amesema watu wanapaswa kuelewa kuwa teknolojia ya mawasiliano ni jambo ya muhimu katika maisha ya binadamu hasa katika sekta ya biashara na usalama nchini.


“Watu wengi wamekuwa wakifanya biashara mitandao huku wengine utumia simu kutuma fedha na wengine ufanya uhalifu wa kimtandao hivyo kama nchi tunatakiwa kujipanga vizuri kudhibiti matumzi mabaya ya mitandao,” alisema.

Hata hivyo amesema katika ziara hiyo wameona uwekezaji mkubwa uliofanyika TCRA hivyo wanaipongeza serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais John Magufuli.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na mabalozi wa Tanzania wanawakilisha nje za Nje walipotembelea mamlaka jijini Dar es Salaam.
 Mabalozi wa Tanzania wanawakilisha nje za nje wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia Maendeleo yaliyofanyika katika mamlaka hiyo.
 Mhandisi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Victor Kweka akiwapa maelezo mabalozi namna ya garai la mambo wanapo angalia masafa ya  mawasiliano wakati walipotembelea Mamlaka hiyo.
Balozi wa Tanzania nchini Sweeden Dkt.Wilbroad Slaa akicgangia katika mkutano wa mabalozi wakati walipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.


from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KO5j32
via
logoblog

Thanks for reading TCRA yawaomba mabalozi kutafuta wawekezaji Viwanda vya kuunganisha simu Janja

Previous
« Prev Post