Ticker

10/recent/ticker-posts

Serikali yadhamiria kumaliza tatizo la Maji Kibondo


Na Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha inamaliza tatizo la maji nchini, Serikali imedhamiria kutumia Shilingi Bilioni 1.2 katika Mji wa Kibondo mkoani Kigoma kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Mabamba-Mkarazi na Kitahana utakaotoa huduma ya maji ya Uhakika kwa wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kitahama, Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso amesema Fedha hizo zimetolewa ili kutimiza ahadi ya Mhe Rais Dk John Magufuli ya kuwapatia wakazi wa Kibondo huduma ya maji.

" Kibondo ni miongoni mwa miji yenye uhaba wa Maji na kwa kutambua hilo tumetoa Bilioni 1.2 kwa mradi wa Mabamba-Mkarazi na tutatoa Bilioni 1.1 kwa ajili ya ujenzi wa mradi mwingine wa maji wa wakazi wa Kibondo.

" Dhamira ya Rais Magufuli ni kumtua Mama ndoo kichwa ni na kama Wizara tunatekeleza maagizo hayo na nimejionea tayari mradi umeanza kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi, kazi iliyobaki ni mkandarasi kumaliza ujenzi wa Vilula vilivyobaki," amesema Mhe Aweso.

Awali Mhe Aweso ameto matumaini kwa wananchi wa Mji wa Mwandiga uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuwa ifikapo mwezi August, Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 za kuanzia kazi ya ujenzi wa miundombinu itakayopeleka huduma ya Maji kwa wananchi kutoka kwenye mradi wa Maji Kigoma Mjini.
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akiwa katika katika kijiji cha Kitahama,Kibondo mkoani Kigoma kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kupitia miradi mbalimbali inayojengwa mkoani humo





from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2jGosdT
via

Post a Comment

0 Comments