Ticker

10/recent/ticker-posts

RAIS WA UTPC AWATAKA WANAHABARI NCHINI KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA(NHIF)

Na Editha Karlo,Kigoma

RAIS wa umoja wa  vilabu vya waandishi wa habari Tanzania(UTPC) Deogratius Nsonkolo ,amewahimiza wanahabari watumie fursa ya umoja wa vilabu vyao, kujiunga na huduma ya mfuko wa  Bima ya afya (NHIF) kwaajili ya kupata kadi za matibabu na kuwa na uhakika matibabu wanapougua wao na familia zao.

Nsokolo ameyasema hayo jana Kigoma mjini wakati akifunga  Kikao kazi cha  wanahabari na viongozi wa mfuko wa bima ya afya ngazi ya Taifa  na mkoani humo lengo la kikao hicho ni kujenga mahusiano ya utendaji kazi baina ya Mfuko wa bima ya Afua Taifa(NHIF)na wanahabari wa Kigoma.

Alisema ni wajibu wa wanahabari kwa kupitia kalamu zao kuelimisha jamii umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanaugua.

"Hata sisi waandishi tunapaswa kuwa mfano katika suala hili la kujiunga na mfuko wa bima ya afya,kunabaadi hawana mikataba  ya kazi kwenye vituo vyao vya wanavyo fanyia kazi hivyo ni vyema tukanyima kwa fedha chache tunazopata tukajiunga kwani ugongwa ukija hauna taarifa unaweza ugumua huna hata mia ila ukiwa na kadi ya nhif unapata matibabu,"Alisema

Alisema inatakiwa sasa klabu za waandishi nchini ziweke mkakati wa kila mwanachama atoe fedha kwa utaratibu utakaokubaliana kila mtu atoe kidogokidogo hadi  kiasi cha fedha sh.76,800  na zipelekwe katika mfuko wa NHIF waweze kupata kadi za matibabu.

 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa bima ya afya NHIF Taifa Anjela Mziray asema NHIF ina mahusiano mazuri na klabu za waandishi wa habari katika Mikoa yote hiyo ni kwaajili ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu hali kama hiyo inachochea wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya CHF au NHIF.

"Niwaombe hata nyie Waandishi tumieni fursa ya Kikoa kujiunga na mfuko wa bima ya afya ,Serikali inataka kila mwananchi apate huduma bora za afya kuanzia vipimo na dawa kwa wakati,athari ya kutokuwa na bima ya afya ni janga kwa familia kukimbiana linapokuja suala la mchango wa kumtibia mgonjwa mfano,tatizo la kusafisha  figo Kwa mwezi unahitaji uwe na fedha si chini ya sh.milioni moja kwa mwananchi wa maisha ya kawaida ataweza?lakini ukiwa na kadi ya bima ya afya una kuwa na uhakika wa matibabu"Alisema

Ofisa Uthibiti na Uhakiki wa ubora NHIF mkoani Kigoma  Dkt . Daniel Kihaya amesema waandishi wa habari  wathubutu kutoa habari zenye kuibua uwajibikaji baina ya watumishi wa afya,mwanachama na huduma za mfuko huo ili,kukomesha tabia ya watumishi wa afya wanaokwamisha dhana ya bima ya afya kwa maslahi yao binafsi.

"Waandishi ni watafiti nyie muwe mnapita pita huko kwenye zahanati na hospital muibue mambo mbalimbali wanayafanya watoa huduma wasiowaaminifu kwa wanachama wa mfuko tukishirikiana tutakomesha tabia mbaya mbaya zote"alisema

Takimu inaonyesha hadi sasa wananchi waliojiunga na mfuko wa bima ya afya ya NHIF na CHF ni 32% kwa nchini nzima,lengo  kufikia 50%ifikapo mwaka 2020 huku Mfuko wa NHIF ukiwa ni miongoni mwa mfuko bora unaotambulika kimataifa kwa utoaji  wa huduma bora ya Afya (ISO ,901/2015) .

 Kaimu Meneja wa NHIF kigoma Emanuel Kileo ataja moja ya matarajio ya kuongeza wigo wa wanachama ni pamoja na ujio wa  uzinduzi wa kampeni ya  Ushirika afya na kusisitiza kutokana na mashirikiano  na vyombo vya habari na wandishi wake watafanikiwa  kuibua na kutokomeza kero ya ulaghai wa utoaji huduma kwa watumiaji wa Mfuko huo.

Meneja mahusiano wa mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Angela Mziray akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi baina ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma na maofisa wa mfuko wa bima ya afya.

Sehemu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma wakisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na maofisa wa mfuko wa bima ya afya (NHIF)



from MICHUZI BLOG http://bit.ly/2Gcvhxg
via

Post a Comment

0 Comments