Ticker

10/recent/ticker-posts

Farasi Kubeba Jeneza la Mzazi Mwenziye na Diddy

Farasi Kubeba Jeneza la Mzazi Mwenziye na Diddy
Kim Porter (47), aliyekuwa mzazi mwenzake rapa maarufu wa Marekani, P Diddy, atazikwa mahali alipokulia, na Diddy amesema atahakikisha anampa maziko yanayomfaa mwanamke huyo ambaye alikuwa ni kipenzi cha roho yake.

Habari zilizopo zinasema Kim atazikwa Jumamosi hii huko Columbus, Georgia, ambako alikulia na kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu mwaka 1988.  Ni huko pia mama yake, Sarah, alizikwa mwaka  2014.

Nyumbani kwa P Diddy wakati wa ibada maalum kwa Kim.

Ijumaa usiku wiki hii marafiki na familia ya Kim watakutana kwa chakula cha usiku kabla ya mazishi yake.

Taarifa zinaongeza kwamba jeneza la Kim litakokotwa na farasi na Mchungaji maarufu T.D. Jakes ataendesha ibada ya kumwombea marehemu.

Jumapili iliyopita Diddy alifanya ibada ya kumbukumbu kwa ajili ya Kim nyumbani kwake Bel Air ambako watu wapatao 100 walihudhuria, ikiwa ni pamoja na mastaa kama Montana, Mary J. Blige na Pharrell.

Kim, Diddy.

Porter alikuwa amefariki nyumbani kwake huko Los Angeles Alhamisi iliyopita akidaiwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na mafua (flu).

Hata hivyo, haijathibitishwa iwapo flu ndicho chanzo halisi cha kifo chake.  Kim alikuwa ametembelea Afrika muda mfupi kabla ya kifo chake na madaktari wanahisi labda aliambukizwa ugonjwa fulani katika safari hiyo.

Sababu ya kifo chake itatolewa, kwa mujibu wa uchunguzi, baada ya wiki nne hadi sita vijazo.