Ticker

10/recent/ticker-posts

DIAMOND HANA TATIZO NA ALIKIBA-; BABU TALE

Hamisi Taletale almaarufu kama Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz na wasanii wote katika label ya WCB hivi karibuni alipata mualiko wa ftari yeye na management nzima ya WCB. Hawakuwa ni WCB pekee tu ambao walialikwa katika hafla hiyo bali na mastaa mbalimbali walipata mualiko huo akiwemo hit maker wa single ya Aje (Alikiba).
Katika hali ya ubinadamu na pasipo na tatizo lolote Meneja wa Diamond (Babutale) alitokea kupiga picha ya pamoja na Alikiba msanii ambaye ana upinzani wa kibiashara na Diamond Platnumz ambaye anasimamiwa na babu Tale.

Picha hiyo ilizua gumzo kubwa katika mitandao ya kijamii kwa mashabiki wa pande zote mbili kuwa na sintofahamu inawezekanaje watu wawili wasiokuwa na mawasiliano mazuri kama wanavyo fahamu wao kuweza kupiga picha!
Babu tale amezungumza na kuweka wazi jambo hilo kuwa msanii wake hana tatizo lolote na mkongwe huyo wa Bongo flavour bali ni upinzani wa kibiashara tu ambao unafaida kwa muziki wa Bongo Flavour na ndio unafanya muziki wa Bonngo Flavour usonge mbele.
Babu tale pia alizungumzia sababu za Diamond kuto hudhuria katika hafla hiyo na kuukanusha ule uvumi ulokuwa ukisema kuwa Diamond hakufika eneo lile kwa sababu alijua Alikiba atakuwepo.
"Ngoja niwatoe hofa watanzania mimi siwezi kuwa na tatizo na Ali hata siku moja, mimi ni mfanya biashara wa muziki, leo niko na Diamond kesho naweza kuwa na ALi. napia niwatoe hofu kuwa hata siku moja nasibu pi hawezi kuwa na matatizo na ALi hizo ni chalenji za kibiashara ambazo zinakuza muziki wetu. Alisema Babu Tale. Msikilize hapa chini.