Na Hamida Hassan
Ukijaribu kufuatilia utabaini kuwa, wengi ambao sasa ni maarufu,
wamefanya mambo makubwa! Walikuwa hawajulikana huko nyuma lakini
walipoingia kwenye muziki, filamu na fani nyinginezo kisha wakafanya
vizuri, walijikuta kwenye orodha ya mastaa.
Kwa hapa Bongo, wapo watu ambao wana majina lakini yawezekana
wasingeingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wale ambao tayari ni
mastaa, wasingekuwa na umaarufu walionao leo.
Ezden Jumanne
Huyu
fani yake ni ya utangazaji. Kwa wale wanaofuatilia mambo watakumbuka
kuwa, kabla ya kuanzisha uhusianao na mtangazaji mwenzake Khadija Shaibu
‘Dida’, hakuwa maarufu.
Walipoanzisha uhusiano ndiyo habari zake na mpenzi wake huyo zikaanza
kuandikwa na kujikuta akijulikana sana. Hata hivyo, utakubaliana na
mimi kwamba, tangu ndoa yao ivunjike, kama vile ameanza kufifia hivi
licha ya kuwa bado anaendelea kufanya vizuri kwenye utangazaji wake
kupitia TV One.
Siwema Edson
Ni
binti wa mjini ambaye inadaiwa anafanya kazi kwenye shirika moja la
ndege nchini. Licha ya vurugu zake alizokuwa akifanya mjini, hakuupata
umaarufu, alipokuja kunasa kwenye penzi la mwanamuziki Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ jina lake likaanza kupaa.
Penniel Mungilwa 'Penny'
Ni
mtangazaji anayeimudu vyema fani hiyo lakini ni ukweli ulio wazi
kwamba, kabla ya kuwa na uhusiano na Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’,
hakuwa akujulikana kivile.
Baada ya kuanza kumuita msanii huyo baby…sweetheart, honey na majina
mengine matam, akaanza kuwa staa. Ila, kuoneshwa kuwa alibebwa na
Diamond, sasa hivi umaarufu wake umepungua tangu waachane.
Moze Iyobo
Dogo
ni dansa wa Mwanamuziki Diamond. Alianza kufanya kazi hiyo muda mrefu
lakini hakuwa maarufu. Jina lake likaanza kupaa baada ya kudaiwa kuwa
anatoka na Aunt Ezekiel.
Baada ya kuvuma kwa tetesi hizo, wengi walishindwa kuamini kutokana
na kwamba, wawili hao hawaendani. Jina likazidi kukua baada ya kuwepo
kwa taarifa kwamba hata mimba ya Aunt ilikuwa ikimhusu.
Hapo ndipo kijana huyu akaanza kung’aa na kuwa maarufu kiasi kwamba sasa hivi huwezi kumtaja Aunt bila Moze.
Malick Bandawe
Ni mwanamuziki, mmoja kati ya waanzilishi wa Kundi la TNG lililokuwa
na maskani yake jijini Tanga. Hakuwa maarufu kiivyo licha ya kwamba
alikuwa akifanya vizuri kwenye muziki.
Alipozama kwenye penzi zito na msanii wa filamu, Rose Ndauka, mara
nyingi alikuwa akiandikwa na kumfanya awe maarufu. Na yeye sasa hivi
kama anapotea baada ya penzi lao kuvunjika.
Bond Suleiman
Fani yake ni utangazaji, anajihusisha pia na mambo ya filamu lakini
baada ya kudaiwa kutoka na Lulu Semagongo kisha kuhamia kwa Wastara
Juma, sasa hivi naye amekuwa staa.
Ni wazi kwamba, kama siyo Anti Lulu na Wastara, huenda angekuwa anajulikana lakini si kwa kiwango cha sasa.
Abdallah Mtoro ‘Dallas’
Ni mfanyabiashara ambaye alikuwa hajulikani kabisa. Upedeshee wake wa
enzi hizo ukamkutanisha na msanii wa filamu, Jacqueline Wolper.
Baada ya wawili hao kuwa wapenzi, jina lake likawa maarufu lakini na
yeye baada ya kuachana na Wolper kisha kudaiwa kufulia, umaarufu
‘kwishinei’.
Faiza Ally
Miongoni mwa mabinti mcharuko kwa sasa mjini, Faiza ni mmoja wao.
Hakuwa na jina kabisa lakini alipodondokea mikononi mwa mwanasiasa
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, habari zao zikaanza kuandikwa.
Hata hivyo, hakuwa maarufu, aliuheshimu uhusiano wao, akaficha makucha. Walipoachana, Faiza akaanza kuonesha yeye ni nani.
Kila mtu sasa anamjua kutokana na tabia zake. Uvaaji wake wa kihasara
ndiyo ambao kwa kiasi kikubwa umemfanya leo hii awe maarufu.
Zarinah Hassan ‘Zari’
Ni ukweli usiopingika kwamba, hapa Bongo mpenzi huyo wa Diamond
hakuwa akijulikana sana. Alipowekeza penzi lake kwa staa huyu kutoka
Tandale, vyombo vya habari vikaanza kumuandama.
Leo hii anaweza kuwa staa ambaye jina lake ni maarufu sana kuwashinda hata baadhi ya mastaa wa kike Bongo.
With my Brothers in Leadership...
-
Asanteni Kaka Zangu,naendelea kujifunza kwenu.
(Mimi,DC Simalenga na DC Mchopanga)
1 week ago
0 Comments