Ticker

10/recent/ticker-posts

GOOD NEWS YA UGENI MKUBWA NDANI YA KENYA....NI HUYU MSANII MKUBWA WA KIMATAIFA..

akon
Mara nyingi mastaa wakiamua kuingia kwenye nchi fulani kwa ajili tu ya kuenjoy huwa wanafanya safari zao kimya kimya ili kuondoa mazingira ya kukutana na misukosuko ya fans ambao labda wangejaa kila anapoenda.. Akon aliwahi kufanya surprise ya hivi Kenya mwaka jana.
Akon aliingia kimya kimya na kuwa sehemu ya mashabiki wa nguvu waliojitokeza kwenye show ya Rapper 2 Chainz iliyofanyika December 2014 Nairobi.
Najua hii inakuwa good news watu wa Nairobi kwa mara nyingine, Akon anarudi wiki ijayo kwa ajili ya fainali za shindano la Airtel Trace Music Star itakayofanyika March 28 Enashipae Resort, Naivasha.
Akon-and-Uhuru
Akon atakuwa na team ya watu watatu ikiwemo Devyne Stephens ambae ndiye aliyegundua kipaji cha Akon kimuziki na kumtoa kwenye game kupitia lebo yake ya UpFront Records.
Mastaa hao ni sehemu ya meza ya Majaji wa shindano hilo.