IMEKULA kwake!
Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa
kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba si mtokaji kwenye misiba ya
wenzake.
Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul
Sykes ‘Dully Sykes’, Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao
walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao
zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile
ambayo itampa ‘kavareji’ kwenye vyombo vya habari.
WASIKIE WENYEWE
“Mimi
nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa
sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha
kwenye media.
“Halafu
akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile
alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya
hapo sikumbuki,” alisema msanii mmoja.
Msanii
mwingine aliongeza: “Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa
tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini
ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji wake.”
Akaongeza tena: “Kama sijasahau hata kwenye kifo cha mwanamuziki wa
Bendi ya Msondo, marehemu Maalim Gurumo hakutokea japokuwa alikuwa
amerudi nchini kutoka nje. Magazeti mliandika kwamba Wema alimzuia
kwenda kuzika. Sasa ni vizuri kweli?”
WANAOTOA POLE KWENYE MITANDAO
Wakati
wasanii hao wakimchana Diamond, wasanii wa filamu, Tamrina Poshi
‘Amanda’, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha wao walisema wanakerwa na
tabia ya baadhi ya wasanii kutohudhuria misiba ya wenzao na kuishia
kutoa pole kwenye mitandao ya kijamii.
Wakizungumza na Amani, wasanii hao walisema imekuwa ni kawaida kwa
wasanii kutohudhuria misibani bila kuwa na sababu na kuongeza kuwa tabia
hiyo si nzuri kwa umoja wao.
AMANDA
“Mfano
mzuri tunauona hapa leo, mwenzetu kafiwa na baba yake ukiangalia
wasanii waliohudhuria wanahesabika lakini nimepata mshangao kwa sababu
rafiki mkubwa wa Dully ni Diamond lakini hapa hajaonekana. Tunaona tu
pole zinaishia kwenye mitandao. Mtu yupo Zanzibar tu hapo na anatupia
picha akiwa na mpenzi.”
BELA NAYE
Kwa
upande wake, Bela alisema alipata taarifa za msiba huo akiwa hospitali
amelazwa lakini akaona ni vema ahudhurie mazishi kwa kuomba ruhusa kwa
daktari pamoja na kuwa hali yake haikuwa nzuri.
“Nilikuwa
nimelazwa na niliwekewa dripu kabisa baada ya kugundulika nina malaria
tano, lakini nikaona siwezi kukosa kuhudhuria msiba kwa sababu marehemu
mzee Sykes mbali ya kuwa baba yetu alikuwa mshikaji wetu sisi wasanii,”
alisema Bela.
BABY MADAHA
“Jamani
hili jambo lisikieni tu kwa watu, mimi sikuamini kwa sababu siku siyo
nyingi Dully aliniambia baba yake anaumwa miguu na walikuwa kwenye
mipango ya kumpeleka India akatibiwe, kumbe baadaye hali ilibadilika
mpaka umauti ukamkuta, nimeumia sana.
“Wasanii tuache ‘u-snich’ (unafiki) kwa sababu wengi wetu wanaishia
kuandika kwenye mitandao tu mi sidhani kama hiyo ni faraja, faraja ni
kumfariji mwenzetu tena kwa ukaribu.”Diamond alipotafutwa kwa njia ya
simu alisema: “Hata mimi nimeumia kwa kifo cha baba’ke Dully lakini si
kwamba sijakwenda makusudi, nilikuwa na dharura.”
Mzee Sykes (pichani) alifariki dunia, Jumapili ya Februari 15 katika
Hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa akisumbuliwa na presha. Alizikwa
Februari 16 katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar.