Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.
Kwa kiasi kikubwa katika suala la
kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga
ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra
shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na
Harusi.
Hata hivyo, kwa wale wanawake
wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea
kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa
kabisa)
1. Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo
(lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya
mwanaume ambaye angependa awe mume wake.Wanawake hawa hujiamini zaidi na
kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe
nazo.
Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi
ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa
kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti
nzuri n.k.
Inaweza kuwa kama mzaha na
ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza
kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile
ambavyo yeye anataka mumewe awe.
2. Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi.
Yupo tayari kuolewa ila si kwa
mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume ana uwezo
kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai
hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya
kifahari.
Hivyo hukazana kusubiri na
kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila
kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.
3. Kutompata Mwanaume Ampendae
3. Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili ni kama tu vile ilivyo kwa
wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na haifai bali tu hadi pale
umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini anakupenda pia.
Wengi katika kundi hili huamini kuwa
mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata
kwenye sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo vya mwanamme awe vipi
havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.
Yeye kikubwa anataka ampate mume
ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini kuwa huyo mume
atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanamke anaamini msingi bora wa
ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe basi! Hana haraka hadi
pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo atakapokuwa tayari kuolewa.
4. Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)
Kuna wale wachache ambao akili
hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala kujitambua ni nini wanataka
ama mwanaume wa aina ipi wanataka.
Akija wa mwenye uwezo atasema nataka
wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa sababu tu hata kama
kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta maendeleo.
Akija wa kabila hii, atasema hapana
hao wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa
kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa.
Hatimaye inaweza tokea muda wa
kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa hata
wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.
5. Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni kweli
Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni
mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata
wote kumtamani.
Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao
huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona ni mzuri mno
hakuna mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili
hufanya kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu
anatakiwa atambue kuwa ana bahati sana.
Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya
juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume
kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.
6. Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.
Wanawake wametofautiana mipangilio
yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri wa kuolewa hutamani sana
kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.
Katika kundi hili umri kuwa mdogo
hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona
mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na
anafaa kuolewa.
Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.
Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.
7. Maradhi hasa UKIMWI
Hili kama lilivyo kwa wanaume -
Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa
mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na mahusiano na hata kuoa na
kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana wanaojitambua kuwa ni
waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na
mtoto.
Wengi sana hukata tamaa na huona ni
kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani
kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.
8. Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya
tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa
na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na
kwao pia.
Hilo linafanya vigezo ambavyo
mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa kutotimiza
yale ambayo yeye binafsi anatarajia.
Wengi hushindwa kutambua kuwa hakuna
maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya maigizo yapaswa
kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi kiigwe na kipi
kiachwe kama kilivyo.
9. Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza
kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe (pengine mama aliteswa sana), na
hata ndugu wa karibu kama vile kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake
anayoijua mwanamke huishi kwa mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na
kuonewa.
- Kuwa na uwezo sana wa
kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile ambalo
anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake anaona
kama ni utumwa.
10. Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale wachache
waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya kuweza kupata
hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi.
Wengi wa aina hii ya wanawake huwa
ni waoga sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi
hata jaribu baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na
uchafu.
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.