Ticker

10/recent/ticker-posts

MUONE HUYU RAPPER ALIVYOMUA MKEWE NA KUJIUA, KISA KIZIMA HIKI !!!

Rapper wa Marekani, Earl Hayes amemuua mke wake Stephanie Moseley aliyekuwa staa kwenye kipindi cha “Hit the Floor” cha VH1 kwa risasi na yeye kujiua kutokana na wivu wa mapenzi.
stephanie-moseley
Stephanie Moseley
Hayes alikuwa ameumizwa na uhusiano wa kimapenzi aliokuwa nao mke wake na Trey Songz. Stephanie Moseley aliuawa nyumbani kwao na mume wake huyo huko Los Angeles.
Hayes45
Hayes
Vyanzo vilivyo karibu Hayes, vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Hayes alitengana na mke wake miaka miwili iliyopita baada ya kugundua alimsaliti na Songz. Walirudiana lakini Hayes hakuwa amepona kidonda cha kusalitiwa na kwenye mazungumzo yao mara nyingi alikuwa akikumbushia suala la Songz.
Trey ametweet:
R.I.P babygirl. Once an angel on earth, now watching over us from Heaven. You’ll b missed but never forgotten. Love
Hayes alimshutumu mke wake kwa kuwa pia na uhusiano na mastaa wengine. Stephanie alikuwa dancer wa waimbaji maarufu wakiwemo Chris Brown na Usher, japo hakuwataja kama chanzo cha mgogoro wao.
Chris-Brown-and-Stephanie-Moseley
Chris Brown na Stephanie
Hayes na Moseley walifunga ndoa mwaka 2008 na marafiki zao wanasema alikuwa akimpenda mno mke wake. Chanzo kingine kimeuambia mtandao wa HollywoodLife.com kuwa Hayes alikuwa anaendelea kumhisi mke wake anamsaliti kabla ya kumuua.
Trey Songz
Kimesema Stephanie alikuwa anataka kumuacha mumewe kutokana na tabia yake ya kumchunga muda wote. Kimeongeza kuwa rapper huyo aliwahi kutishia kujiua kama mke wake angemuacha na kweli Stephanie alikuwa amuache miezi miwili iliyopita.
Katika hatua nyingine, mtandao wa TMZ umedai kuwa bondia Floyd Mayweather alikuwa akiwasiliana na Hayes aliyekuwa rafiki yake kupitia mtandao wa video wa FaceTime na alishuhudia yote yaliyotokea.
Rapper huyo alimpigia Floyd kutumia FaceTime Jumatatu asubuhi akiwa amekasirika kutokana na madai kuwa mke wake si mwaminifu. Kwa mujibu wa vyanzo, Earl alisema angemuua mke wake. Bondia huyo alijitahidi kumuomba asichukue uamuzi huo lakini alishindwa.
Floyd hajasema alichoona lakini amekubali kuwa alikuwa shuhuda na alisikia kila kitu. Floyd yupo kwenye wakati mgumu kutokana na tukio hilo.