Ticker

10/recent/ticker-posts

WAFAHAMU WATOTO MAARUFU WENYE USHAWISHI ZAIDI DUNIANI.

maddie-ziegler
Maddie Ziegler ni msichana wa miaka 14 ambae kwa mara ya kwanza alionekana kwenye TV Show iliyokua ikiitwa Dance Moms. Umaarufu wake ulizidi kuongezeka mara baada ya mtoto huyo kujiingiza kwenye fani ya uchezaji muziki (Dancer)  kama umeiona Chandelier ya Sia utakua umemuona mtoto huyu michezo aliyotisha nayo humo.
Ziegler alikua jaji kwenye msimu wa sita wa shindano la So You Think You Can Dance:
malia-obama-300x400
Michelle Obama anatajwa kama moja kati ya wanawake wahamasishaji na wapenda maendeleo kwa sasa anaungana na binti yake Sasha kuendelea kuelimisha wanawake waelimike, Malia Obama anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha Havard.
Barack Obama ambae ni Baba yao mzazi ameshikiria rekodi ya kuwa Rais wa kwanza mweusi nchini Marekani..
Malia na Sasha Obama pia hawajasahaulika kwenye orodha hii ya mastaa wenye umri mdogo na ushawishi mkubwa duniani.
Zara_Larsson_Stavernfestivalen_(203836)
Miaka nane sasa baada ya ushindi wake kwenye Tamasha la America’s Got Talent, Zara ni mmoja kati ya watoto wanaosumbua sana kwenye muziki wa Pop. Kwa miaka ya hivi karibuni Zara amezidi kujizolea umaarufu baada ya kusikika kwenye ngoma kadhaa zikiwemo “Never Forget You” aliyoshirikishwa na MNEK na ile ngoma ya kombe la Euro “This One For You” ya mtu mzima David Gueta.
“Ain’t my fault” ndiyo ngoma ya mrembo Zara iliyoko kwenye chati kwa sasa kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kijamii ngoma hiyo imetajwa kama ngoma inayomjenga zaidi mtoto wa kike na wanawake wengi ambao wamepata nafasi ya kuisikiliza.
jaden
Mtoto wa muigizaji Will Smith ambae haishiwi vituko na moja kati ya maajabu yake ni uvaaji wake wa mavazi yake ya kike ambayo yamefanya jina lake kuzidi kutajwa kwenye Industry ya Fashion…
Akiwa na umri wa miaka 18 Jaden Smith tayari amezindua brand yake ya mavazi inayoitwa MSFTSrep nguo maalum kwa wasichana wenye tabia za kiume (TomBoy) au wavulana wanaopenda kuwa na muonekano wa kike.
kjenn
2016 umekua ni mwaka wa kismati kwa girlfriend wa mnyamwezi Tyga kwani Licha ya Staa huyo wa TV Show ya “Keeping Up With The Kardashians” kumiliki mijengo na magari ya kifahari mrembo Kylie Jenner anamiliki kampuni yake ya vipozi (Kylie Cosmetics) pia ameonekana kwenye kurasa mbalimbali za majrida makubwa likiwemo Allure Magazine.