15034852_1198217740265763_8711447471730982912_n
Snura anasema kipindi ambacho wimbo wake Chura unafungiwa kilikuwa cha misukosuko lakini aligoma kukata tamaa.

Akizungumza na mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove, Snura alisema neno kukataa tamaa halipo kwenye orodha ya msamiati wake.
“Kwenye suala la kukataa tamaa kwangu halipo,” alisema. “Na kama ningekuwa ni mtu wa kukataa tamaa ningekata tamaa kwenye Chura, lakini sikukataa tamaa hadi kuhakikisha nairudisha na masekeseke ya chura yale yaliyotokea yangenikatisha tamaa. Nimekutana na mambo mengi sana kuhusiana na chura,” alisema.
Snura anasema hasara iliyopatikana kutokana na kufungiwa kwa chura ilikuwa kubwa kwakuwa ilikuwa na dalili za kuwaingizia fedha nyingi kwenye Youtube ukiachilia deals zingine za show.

SHARE 

TOA MAONI YAKO HAPA

 
Top