Ticker

10/recent/ticker-posts

Je, Kujamiiana Huondoa Msongo wa Mawazo Kwa Wanawake?

UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu cha State cha jijini New York nchini Marekani unaeleza kuwa manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea msongo wa mawazo.

Pia, watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.

Hali hii wamesema wataalam hao kuwa inatokana na manii kuwa na kemikali ambazo humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu, huchochea mtu kupata usingizi na huwa na angalau aina tatu za kemikali za kuondoa msongo wa mawazo (anti-depressants).

Utafiti huo uliofanywa kwa kuwahoji wanawake 293 kwa kufuatilia maisha yao ya kujamiana dhidi ya afya za akili zao. Manii huwa na mchanganyiko wa kemikali aina ya cortisol ambayo huongeza upendo, kemikali aina ya esterone na oxytocin ambazo zote humfanya mtu kuwa vizuri  kihisia.

 Pia, huwa na homoni aina za ‘thyrotropin releasing hormone’, ambayo huondoa msongo wa mawazo, melatonin ambayo huchochea usingizi na serotonin ambayo ni homoni inayoondoa msongo wa mawazo.


Kutokana kuwapo kwa mchanganyiko wa kemikali na homoni hizo kwenye manii

Matokeo ya utafiti

Matokeo muhimu ya utafiti huu ambao umechapishwa katika jarida la ‘Archives of Sexual Behaviour’ ni kwamba hata baada ya baadhi ya watafitiwa kuongeza kiwango chao cha kujamiana, wale ambao walikuwa hawatumii kinga yoyote walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao walikuwa wakitumia kinga kama kondomu wakati wa kujamiana.

 Pia, wanawake hawa ambao hawakutumia kinga walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawakushiriki tendo la ndoa kabisa.

Watafiti hao wamesema siyo tu kujamiana huongeza furaha kwa mwanamke na hivyo kumwondolea msongo wa mawazo, bali kiwango cha furaha pia huendana na wingi wa manii katika mili yao.


Hata hivyo, ushauri wa kitaalamu ni kuwa utafiti huu usiwe chanzo cha watu kufanya mapenzi bila kinga bali uwe chanzo cha kufanya mapenzi salama na mwenza unayemwamini.

Pia, tunakemea na kupinga wale wote wanaofanya vitendo vya usagaji kwani ni hatari kwa afya zao kwani ni chanzo kimojawapo cha magonjwa ya akili. Wiki ijayo tutakuletea mengi kuhusu uhusiano kati ya usagaji na ugonjwa wa akili.