Ticker

10/recent/ticker-posts

MAPENZI:HAYA NDIYO MAMBO MUHIMU AMBAYO MWANAMKE ANAHITAJI KUTOKA KWA MWANAUME

Image result for black couples with friends
Ni mara nyingi sana tunasikia wanaume wakisema
“mke wangu wala huwa simuelewi”
Ni kweli wanaume tunahitaji kujua baadhi ya vitu kuhusu wanawake ili tuweze kuwafahamu zaidi.
Je ni mambo gani wanawake huhitaji kutoka kwa mwanaume?

Wanawake huhitaji mwanaume anayesikiliza zaidi kuliko kutoa jibu tu.Wanaume ni watu wa kutia majibu (problem solvers).
Image result for black couples with friends
Pia wanaume hujitahidi kuhakikisha mambo yanakuwa sawa kwa kila mmoja bila kusahau masuala ya mahusiano hata hivyo kuna wakati na muda wa kutoa suluhisho na pia kuna wakati ambao mwanaume anatakiwa kusikiliza tu kwa mwanamke.
Kama mke moja kwa moja amekuomba usaidie kutoa sukluhish la jambo Fulani hapo haina tatizo moja kwa moja toa jibu an fanyia kwazi.
Ila kama mke anakueleza kitu ambacho amekutana nacho iwe kazini au akiwa na watoto usitoe suluhisho kabla ya kumsikiliza kwanza.
Wanawake wanahitaji kubwa la kutaka kusikilizwa na hii ndiyo tofauti kati ya mwanaume na mwanamke, wanaume hutumia ubongo tu hata bila kuongea kuhakikisha anapata tatizo la issue zake wakati mwanamke hulazimika kuzungumza na kusikilizwa ili kupata jibu laissue yake.
Kama mwanaume hutumii muda ku-discuss mambo na mke wako hiyo siyo nzuri ndiyo maana anaweza kutumia muda wake kuongea na rafiki zake kwenye simu kwa sababu hujafanikisha hitaji lake la kusikilizwa.
Mwanaume unapoongea na mwanamke hakikisha:-
Unapoongea naye kwanza unamwangalia usoni (eye contact) ili ajue unamsikiliza
Anapomaliza kuongea hakikisha unaonesha ulikuwa unamsikiliza hasa kwa kurudia yale ameongea kwa mfano unaweza kusema, “kwa hiyo ulikuwa unaniambia ………”
Then muulize yeye alikuwa anafikiriaje kupata jibu la hiyo issue yake kabla wewe kutoa jibu.
Kufanya hivyo kutaonesha unajali sana hisia zake hasa suala zima la kusikilizwa na pia itamsaidia yeye mwenyewe kuangalia ni jinsi gani anaweza kuhusika kupata jawabu la issue aliyokuwa anakueleza.
Wataalamu wanasema mwanamke kawaida huongea maneno 45,000 kwa siku na mwanaume maneno 15,000 kwa siku hivyo ukiwa unamkatisha kuongea na kudakia kwa kutoa jibu bila kumsikiliza kisaokolojia una muumiza na itabidi atafuta mtu mwingine wa kuongea naye.

Wanawake wanahitaji mwanaume anayemuhitajiWanawake wanapenda kuona wanahitajiwa na mwanaume.