Ticker

10/recent/ticker-posts

KALI YA MWAKA:SHILINGI MILIONI ZAIDI YA 33 ZATUMIKA KUNUNUA JINA TU LA MTOTO!..HII SI KUFURU?CHEKI TU UJIONEE

African American family at homeUlishawahi kujiuliza jina lako lina maana gani au limetokana na nini? wengi tumekuwa na majina ambayo hatujui maana yake na mengi yakiwa ni common, lakini kuna mengine ambayo ni ya kipekee kwa mfano majina ya watoto wa mastaa wa Marekani Kim Kardashian anayeitwa ‘North West’na mtoto wa Beyonce ‘Blue Ivy’, ni majina ambayo inasemekana hayajawahi kusikika sehemu nyingine.

Kampuni moja huko Sweeden ya  Erfolgswelle, ina uwezo wa kubuni jina la mtoto wako ambalo linakuwa la kipekee na huwezi kulikuta sehemu nyingine duniani, ambapo team ya watu 31 hukutana na ndani ya masaa 100 jina hilo linapatikana, awali yanaletwa majina 15 yenye hati miliki na kukaguliwa na wataalam wanne ili kuthibitisha jina hilo halifanani na jina lingine wala kutumiwa na mtu mwingine.
Kabla ya kusajiliwa jina hilo linaangaliwa katika tafsiri kumi kuhakikisha kuwa halitafsiriki kwenye lugha yoyote ile wala halina maana ya kitu chochote, baadae unafanyika utafiti wa kuangalia soko la jina hilo ambapo hujaribishwa  kwa kundi la watu 780, ili kuangalia kama watalipenda kabla ya kulipitisha na kulisajili kisha kulipa kiasi cha dola £21,000 ambazo ni zaidi milioni 33 za Kitanzania.