Ticker

10/recent/ticker-posts

Shaffih Dauda Afunguka: Hii ndio Afrika, Kocha Anakupa Ubingwa Leo Alafu Kesho Unamfukuza

Shaffih Dauda Afunguka: Hii ndio Afrika, Kocha Anakupa Ubingwa Leo Alafu Kesho Unamfukuza

Afrika bado tunafanya mambo yetu kivyetu vyetu! Timu imefuzu Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF bila kucheza mechi hata moja ya Nusu Fainali.

Ni Afrika ambapo RS Berkane ilipewa alama tatu za mezani baada ya mechi kushindwa kuchezwa kutokana na migogoro ya kisiasa. Mchezo wa marudiano, USM Alger walisafiri hadi Morocco lakini hawakuingiza timu uwanjani. Hiyo ndio Afrika!

Huku Tanzania timu imechukua ubingwa halafu kesho yake inatoka taarifa kocha anaondoka! Afrika hiyo. Kuna mambo yanafanyika unabaki kinywa wazi.

Wenzetu wanaofanya mambo kwa kuzingatia weledi wameweza kutofautisha hisia na uhalisia. Pamoja na kuendelea kuhubiri kuhusu weledi lakini nchi nyingi za Afrika tunafanya mambo yetu kizamani.

Inathibitika kwamba tunafanya mambo bila kuzingatia weledi pale inakuja jambo la kimaamuzi, maamuzi mengi huwa yanafanyika pasipo weledi. 

Post a Comment

0 Comments