Ticker

10/recent/ticker-posts

Hospitali Binafsi Zaanza Kupokea BIMA za Afya za NHIF

Dar es Salaam. 
Baada ya wagonjwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kusitishiwa huduma kwa hospitali binafsi, baadhi ya hospitali zimeanza kutangaza kurejesha huduma kwa wanachama hao.
Kiini cha wanachama wa NHIF kusitishiwa huduma, ni Chama cha Watoa Huduma Binafsi za Afya nchini (APHFTA), kutangaza mgomo kikishinikiza kutokubaliana na matumizi ya kitita kipya cha mafao ya gharama za huduma 2023 kilichotolewa na NHIF, wakidai gharama zilizokokotolewa kwenye kitita hicho, ni hasara kwao

Post a Comment

0 Comments